Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Mwabukusi amesema watanzania tuna wajibu wa kikatiba wa kulinda rasilimali za nchi hii. Waziri Masauni na Nape waache kutisha watu, na kwamba yupo tayari kupambana nao kisheria, akisema kuwa mkataba ni wa kijambazi, hataruhusu aina hii ya mkataba kufanya kazi nchini.
Mwabukusi ameongeza kuwa hakuna mwenye risasi ya kuua mawazo na dhamira zetu, kwa njia yoyote watakayoamua kutukabili, kila tendo ovu watakalopanga dhidi yetu litajibiwa kwa njia ileile. Akisema kuwa yeye sio mhaini, ataripoti polisi (wameniita) na nimesoma katiba, kila anayesapoti mkabata huu ni mwizi.
Mwabukusi aongeza kuwa, kuna watu wanasema kesi ipo mahakamani, kilichopo huko ni kutafsiri mkataba, huku mtaani tutaendelea kuwawajibisha waachie ngazi. Sisi tumekuja kwa kuungaunga hapa, hatujahongwa na mtu yeyote, kama yupo wamtaje.
Mwabukusi ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo unaofanyika leo Julai 12, 2023, akiwa na Dr. Slaa, Wakili Madeleka na Askofu Mwamakula.
Pia soma: Wakili Madeleka: Waziri Masauni ana wajibu wa kutekeleza majukumu ya kisera sio kiutendaji. Aache kutisha watu, hajawahi kuwa Mgambo au Sungusungu