upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake amechukuliwa kwa nguvu na Watu wasiojulikana ambao walikuwa wamebeba silaha na ripoti zinadai tukio hilo limetokea February 20,2025 saa saba mchana katika Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa ripoti za Mashuhuda Kijana huyo aliyekuwa anaendesha pikipiki alipambana sana kuomba msaada lakini Watu hao waliokuwa kwenye Noah nyeusi walitoa silaha ikiwemo bunduki na bastola hadharani na ikapelekea Watu waliokuwa karibu washindwe kutoa msaada.
Watu mbalimbali wamepaza sauti zao mitandaoni wakitaka Mamlaka zitolee ufafanuzi tukio hilo, Rais wa TLS Wakili Boniphace Mwabukusi amesema
"Tunataka Polisi watuambie hili ni zoezi la ukamataji? au ni kiburi cha utekaji baada ya kukosekana kwa hatua thabiti za kuzuia uharamia huu? nadhani sasa hapa tutapata majawabu mara moja "