Mwadui FC yamumunywa na Simba SC Kambarage, Mwadui 0-3 Simba

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakuu wa JF
Lile treni lililokatika breki Simba SC linaendelea na safari. Leo hii litapita katika uwanja wa CCM Kambarage kukipiga na Mwadui FC.

Timu bora kabisa chini ya kocha Omog na msaidizi wake Mayanja iliwasilisi majuzi mjini Shinyanga na kuweka kambi hapo kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Mwadui FC.

Awali mchezo huo ulikuwa upigwe katika Uwanja wa Mwadui Complex,utafanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Kikosi cha Simba kikiongozwa na wachezaji wenye vipaji na viwango vya kimataifa, Mzamiru Yasini, Shiza Kichuya, Zimbwe Jr Tshabalala na Ibra Ajib kipo katika ari kubwa.

Mechi hii itarushwa live kupitia Azam TV na kutangazwa na vituo vya TBC One na Uhuru FM.

Kwa hapa JF nitakuletea moja kwa moja kwa msaada wa Azam TV.

MATOKEO: Mwadui 0-3 Simba



SIMBA NGUVU MOJA
 
Kama ada ni speed ya 4G kwenda mbele

Mnyama mkali kuliko wote mwituni
 
ile Habari yenu ya kupanda ndege naskia kuna TV station waliweka kama Habari ya kitaifa hivi walikuwa Na maana gani
 
tutarajie nini kutoka kwa straika lenu hatari la kimataifa mr mavugo?
 
Simba atashinda tu ata na mechi ya stand ratiba imewanyonga stand make wanacheza mechi kesho pwani,jumatatu wanageuza kisha jumatano mechi.
 
Simba atashinda tu ata na mechi ya stand ratiba imewanyonga stand make wanacheza mechi kesho pwani,jumatatu wanageuza kisha jumatano mechi.
Mmeshaanza kutafuta visababu.. Hii ratiba ilitoka wiki kadhaa kabla ya ligi kuanza.. Kwanini hamkusema mapema?.. Mnyama huyu hakuna wa kumzuia kumchukua mwali.
 
Mmeshaanza kutafuta visababu.. Hii ratiba ilitoka wiki kadhaa kabla ya ligi kuanza.. Kwanini hamkusema mapema?.. Mnyama huyu hakuna wa kumzuia kumchukua mwali.
Mimi nimesema tu kama mawazo yangu jinsi stand atakavyoweza kuathirika na ratiba mwishoni ma round ya kwanza.Kwamba alitoka shinyanga kisha mbeya,morogoro,pwani-shy tarehe 2 then mtwara tena tarehe 6.
 
Mkuu sembo umerudi pori tena?tupe tathmini
Mkuu.. nipo mjini.. Hawa Mwadui ni wetu kabisa.. Hebu cheki takwimu hizi;

1. Sisi.
Idadi ya mechi tulizocheza: 11
Tumeshinda: 9
Tumefungwa: Hakuna
Sare: 2
Magoli tuliyofunga: 21
Magoli tuliyofungwa: 3 [ya halali 2]
Nafasi katika msimamo wa ligi: Kama Kawaida [Wa kwanza]

2. Wao.
Idadi ya mechi walizocheza: 11
Wameshinda: 3 tu
Wamegongwa: 4
Sare: 4
Magoli waliyofunga: 9 tu
Magoli waliyofungwa: 10.
Nafasi katika msimamo wa ligi: 11
 
Simba TAIFA KUBWA, tuko pamoja. Mechi hii lazima tulipe kisasi maana Julio alicheza sana alipotufunga msimu uliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…