Mwajiri wako anapokupangia Mshahara hakufikirii katika haya

Mwajiri wako anapokupangia Mshahara hakufikirii katika haya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Hili uliweke akilini mwako kabisa mapema ili baadaye usiyejekulia Lia Kama mtoto.

Mwajiri wako anapopanga Mshahara wako kitu anachokiwaza ni kupata faida maradufu. Pia anawaza ni namna gani utamsaidia kupata faida kubwa zaidi na kufikia malengo yake, na sio kuwaza kukusaidia.

Wakati wewe unamuomba msaada akupe KAZI kumbuka yeye hakusaidii Ila atakuamrisha umsaidie yeye(boss wako) ili apate faida kubwa nawe ujipatie walau.

Mwajiri anapokupigia Hesabu ya Mshahara anakuchukulia wewe Kama wewe na wala haiingizi wala kuzingatia kuwa Una familia sijui mke na watoto watatu. Hilo liweke kichwani.

Hivyo ukiomba kazi jua kabisa majukumu na mahitaji yako ya familia hasa nahitaji ya ziada hayapo kwenye Akili ya Boss wako.

Yeye atakachowaza na Pesa ya Kula, nauli na Kodi ya nyumba basi!

Hayo yako ya kusema unasomesha wala hayamuhusu, usije ukafikiri kuna Boss anayepiga Hesabu ya Mshahara wako ili upate akiba labda ujenge Nyumba nzuri, Hilo wala halipo kwenye Akili yake.

Sijui ununue Gari, au uvae vizuri hayo yote Mwajiri wako hayafikirii.

Unapolipwa Mshahara ni Kwa ajili yako sio ili uweze kuishi na kumtumikia Boss wako na sio ili uwe huru na kujitegemea.

Kuna rafiki yangu, Muha mfanyabiashara alikuwa akipenda kuniambia kuwa yeye Kwa vile hajasoma na aliishia Darasa la tano aliapa kuwa kamwe hawezi kuajiriwa Kwa sababu anajua fika kuwa hatalipwa zaidi ya Laki Tano. Hivyo ni Bora ajiajiri tuu hivyohivyo, akalima Nyanya miaka hiyo akapata pesa nzuri Kwa sasa anaangalau.

Ajira ni nzuri Kama unapata kiwango Fulani cha pesa, Kwa matumizi Standard walau Take home iwe 600,000/= yaani Kwa siku elfu 20. Hiyo ni Kwa mtu asiye na Gari na mwenye maisha ya kubana matumizi.

Vinginevyo Kwa mtu mwenye malengo makubwa Kama atalipwa chini ya hapo basi hawezi kwenda popote.

Jumapili njema.
 
Kuna Ukweli Mchungu Hapa na inabidi waajiriwa watiemo Ukweli huu akilini.

Kwa wanaume:

Kabla hujaoa Jiulize mapato Yako yanatosha wewe mwenyewe kujikimu, kukimu Wazazi na Wakwe?

Kisha kubaliana na Mshahara wa Mwajiri mapema.

Sio unakubali Mshahara halafu unaoa unaona Mshahara hautoshi unaanza kumsumbua Mwajiri akuongezee.. asipokuongezea unaanza kumuibia na kumuharibia kazi.
 
Mshahara umetengenezwa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha unakidhi mahitaji yako na sio maendeleo. JOB - Just Over Broke.
Kwa hiyo usitegemee mshahara kuja kukutoa kimaisha.
 
Mshahara umetengenezwa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha unakidhi mahitaji yako na sio maendeleo. JOB - Just Over Broke.
Kwa hiyo usitegemee mshahara kuja kukutoa kimaisha.

Wangapi wana mishahara na wanatoka kimaisha mtu anayepokea take home 20M unamwambiaje hiyo story yako?
 
Back
Top Bottom