Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Sina maneno mangi naomba niwakumbushe jambo waajiriwa.
Nambari 1: Kama uliweza kuajiriwa ni vyema ukatambua kuwa unaweza kufukuzwa kazi pia.
Nambari 2: Ukifa, ukistaafu, ukiacha kazi, ukihamishwa, ukipunguzwa kazini, ofisi unayofanyia kazi haitafungwa.
Itaendelea kama kawaida na itastawi kama kawaida, hivyo usijidanganye au usidanganywe kuwa wewe ni mtu muhimu hapo ofisini.
Serikali au mkurugenzi mwanzilishi ndio watu muhimu kwenye hiyo ofisi maana hawafukuziki.
Ukizingatia hayo mambo mawili utapata afya katika maisha yako baada ya kazi yako kumalizika hapo ulipoajiriwa.
Stori fupi kidogo
Kuna askari polisi mmoja Kahama aliwasaidia BARRICK (ACACIA) kuokoa Lori la makinikia ambalo watu walikuwa wanalitorosha.
BARRICK wakampa zawadi ya fedha kidogo na kumpa offer ya kumwajiri. Jamaa alipoona mshahara mnono akapiga kalamu chini upolisi na kuwa mlinzi wa mgodi.
Siku moja akiwa main gate, gate number 2 au 3 hivi sikumbuki vizuri ila ni kati ya yale mageti 2 ya katikati ndani ya jengo la utawala. Jamaa alishitakiwa kosa la kukagua vibaya watumishi, ofisi ikamfukuza.
Alilia kama mtoto huku akikumbusha kontena aliloliokoa hata hivyo kilio chake kiligonga mwamba akafukuzwa.
Waajiriwa acheni tabia za uchawa, fanya kazi uliyoajiriwa tu na ile ya ziada uliyopewa na bosi wako.
Kimbelembele kitawaua na pressure mkistaafu.
Nina stori nyingi ila hiyo moja inatosha kwa leo.