SI KWELI Mwaka 1973 viwanja vya mnazi mmoja zilikusanywa Land Rover takribani 350, na Baba wa taifa Mwalimu Nyerere

SI KWELI Mwaka 1973 viwanja vya mnazi mmoja zilikusanywa Land Rover takribani 350, na Baba wa taifa Mwalimu Nyerere

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu Salaamu, naomba msaada kufahamu uhalisia wa hii picha niliyokutana nayo mtandaoni ikidaiwa kuwa Mwaka 1973 viwanja vya mnazi mmoja zilikusanywa Land Rover takribani 350, na Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, uhalisia ni upi katika hili wakuu?

IMG_20241013_142937_769.jpg
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa tovuti ya ofisi ya waziri mkuu inaelezwa kuwa Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba, 1980 na mara ya pili kuanzia tarehe 24 Februari, 1983 hadi tarehe 12 Aprili, 1984 alipofariki kutokana na ajali ya gari mkoani Morogoro.

Hayati Edward Sokoine katika kipindi chake cha kuwa waziri mkuu alisifika kwa uadilifu wake, uchapa kazi pamoja na kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma ambapo mnamo Aprili 5, 1983, Mwalimu Nyerere alizindua kampeni ya kupambana na wahujumu uchumi kampeni ambayo ilisimamiwa na kutekelezwa na Waziri Mkuu Sokoine.

Kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine kilichotokea aprili 12, 1984 kilileta majonzi makubwa kwa watanzania kutoka na ari ya uchapakazi pamoja na kuleta usawa kwa wananchi kwa kuhimiza maendeleo kwa wote.

Kumekuwepo na picha inayosambaa mtandaoni inayoonesha msafara wa magari aina ya LandRovers huku pembeni ya barabara kukiwa na watu wakilaki msafara huo, ikidaiwa kuwa ni mwaka 1973 viwanja vya mnazi mmoja zilikusanywa Land Rover takribani 350 na aliyeanzisha alikuwa ni Baba wa taifa Mwalimu Julius K. Nyerere huku machapisho mengine yakihusisha picha hiyo wakati wa kifo cha Hayati Sokoine.

Je, ni upi uhalisia juu ya picha hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini kuwa picha hiyo haihusiani na kile kinachodaiwa kuwa yalikusanywa magari aina ya Land Rover takribani 350 na kuwa aliyeanzisha tukio hilo alikuwa ni Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, Picha hiyo ilichapishwa katika maeneo mengi mtandaoni ikionesha kuwa sehemu ya matukio kuelekea mazishi Hayati Moringe Sokoine.

Mnamo Aprili 12 2021 Gazeti la Nipashe kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook ulichapisha picha hiyo pamoja na picha nyingine likieleza kumbukumbu ya Matukio katika picha mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Nyerere, Hayati Edward Sokoine, pia picha hiyo ikiambatana na picha nyingine ilitumika na Millardayo.com akiripoti Familia ya Hayati Sokoine, kuandaa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 37 tangu afariki.

Kadhalika mnamo februari 17, 2024 kupitia ukurasa wake Rasmi wa X Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichapisha picha hiyo ikiwa na maelezo haya,

“Kumbukizi ya mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Moringe Sokoine ukipitishwa katika Barabara ya Uhuru, Arusha kuelekea Monduli kwa ajili ya mazishi. Miaka 40 baadaye barabara hiyo imetumika tena kupitisha mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ukisafirishwa kwenda Monduli kwa ajili ya mazishi”
Back
Top Bottom