Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
NIWAKUMBUSHE KUFUFUKA KWA CHADEMA MWAKA 2008.
Leo 11:02am 19/03/2022
Mwaka 2008,Katibu Mkuu akiwa Daktari Wilbroad Slaa,Chadema ilifufuka baada ya kutokea kashfa ya "Richmond" na kuendesha "Operation Sangara" nchi nzima, mikutano yao ilivutia watu wengi kwa hoja zao motomoto za kashfa ya Epa,Meremeta na Richmond,nami nilivutiwa sana nikachangia 10,000 japo nilikuwa mwanaCCM na kwa hakika tuliona effect yake kwenye uchaguzi wa 2010 na tukaendelea tena Mwaka 2013 na 2014 Chadema ikaibuka tena na kashfa ya Escrow,pesa zilichukuliwa bank kwenye sandarusi,mikutano hiyo ya Chadema iliamsha hisia za Wananchi ikawa ukivaa sare za CCM unapigwa au unakimbizwa kama mwizi mtaani,
Shukrani kwa uteuzi wa John Pombe Magufuli kugombea 2015,uchaguzi ulikuwa mgumu 2015 ilifikia wakati taarifa ya habari watu walisubiri mafuriko ya Lowassa tu na yalipopita watu walitawanyika bar,hawakutaka kabisa kusikia taarifa ya habari inayohusu mgombea wa CCM,hiki ndio kilimfanya mgombea wa CCM kujibadili na kuwa mpinzani,CCM ikaanza kutumia slogan ya "Magufuli 4 Change" na Magufuli mwenyewe alianza kutembea kwenye sera za Wapinzani,Wananchi hawakutaka tena kuisikia CCM walitaka kusikia jina la Magufuli tu,na kwa hakika Wananchi walichagua jina la Magufuli awe Rais wao na sio CCM,
Baada ya Rais Magufuli kuingia alianza kuibadili CCM kuwa safi kwa kufukuza Mafisadi yote,ndipo Wananchi wakarudisha moyo wao kwa Chama Chao Cha Mapinduzi,CCM ikashika hatamu tena katika Awamu ya tano,lakini kwa mapenzi yake,Mungu akamtwaa Rais Magufuli,sasa tupo Awamu ya sita ambayo imeanza kufanana na Awamu ya nne,Je Chadema itarudia historia yake toka operation Sangara na kashfa ya Epa,Meremeta na Richmond na Mwaka 2014 kutoka na kashfa ya Escrow,muda ni Mwalimu, tusubiri tuone ya Chadema hii ya Mbowe.
Soma
#KuelekeaUchaguziMkuu2025.