Mwaka 2018 ulikuwa wa Harmonize, 2019 utakuwa wa Mbosso na Marioo

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636
Mwaka 2018 ndio unaishia hivyo na kwenye kiwanda cha burudani haswa bongofleva tumeshuudia mengi yakukumbukwa.

Kikubwa zaidi ni msanii Harmonize kufanya maajabu na singo yake KwaNgwaru, hakuna atakaebisha Kwangwaru imekuwa ni wimbo bora kabisa kwa Tanzania na East Africa na Harmonize amegeuka kuwa msanii mwenye influence kubwa sana kwenye muziki wa bongo.

Tukiangalia kwenye mwaka unaokuja, naona utakuwa mwaka wa wasanii awa wawili Mbosso na Marioo vijana wenye vipaji vikubwa na waliokuja na taste mpya kwenye bongofleva.. Nategemea kuona makubwa sana kutoka kwao na bongofleva itegemee mengi kutoka kwao.

Mengine, tutaona vita kubwa sana kwenye biashara ya muziki haswa kutoka kwa Clouds Media vs Wasafi huku Clouds ikiendelea kutawala upande wa radio na Wasafi wakitawala kwenye Tv mwisho wa siku matamasha ya hizi pande mbili yataendelea kuchuana sana na pengine kutaleta mgawanyiko mkubwa kwenye sanaa.

Kuhusu sanaa kuzaliwa upya?
Yes tutaona mabadiliko mengi kwenye biashara ya burudani yakiletwa na Wasafi na social media.
 
Dogo Aslay huu ndo ulikuwa mwaka wake,katoa nyimbo nyingi kama 8 na zote kali na zimehit
 
Mwaka 2019 ni wangu aiseeh..
Kuanzi mwaka 2000 watu mnajigawia miaka tu.
Huu 2019 na mimi najipa..utakuwa wangu tu
 
Dogo Aslay huu ndo ulikuwa mwaka wake,katoa nyimbo nyingi kama 8 na zote kali na zimehit
Aslay mwaka ulioisha haukuwa mzuri sana kwake, ni kama amefika sehemu amegota aendi mbele wala harudi nyuma. Akijipanga upya akubali kupinduka kidogo atatisha sana next year.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…