Uchaguzi 2020 Mwaka 2020 ni mwaka wa kuiadhibu Serikali iliyoko madarakani

Uchaguzi 2020 Mwaka 2020 ni mwaka wa kuiadhibu Serikali iliyoko madarakani

mcrounmj

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2016
Posts
380
Reaction score
889
Ni matumaini yangu wajumbe mko Poa mkivuta upepo mwanana. Ni miaka mitano tangu Serikali dhalimu ya awamu ya tano iingie madarakani.

Pamoja na mambo mazuri ambayo yamefanyika katika awamu hii, yapo mambo ya kijamii ambayo eidha yamebakia palepale au yamerudi nyuma hatua kadhaa.

Mishahara ya wafanyakazi wa umma kwenye kada mbalimbali imebakia palepale. Katika kipindi cha miaka 5 hapakuwa na nyongeza ya mishahara, hapakuwa na kupanda madaraja pia hata madai ya wafanyakazi hayajatekelezwa.

Miaka mitano ya serikali hii ajira HAKUNA! Tulizoea hapo kabla vijana waliohitimu kada za afya na ualimu, ajira ilikuwa uhakika. Tangu serikali hii iingie madarakani wahitimu wa kada mbalimbali wameongezeka mtaani. Vijana hawa wameendelea kuwa mizigo kwa familia zao, licha ya kutumia muda na mali katika masomo yao.

Ni katika mazingira haya serikali ya awamu ya tano imeelekeza rasilimali za taifa katika ununuzi wa ndege na ujenzi wa flyover, vitu ambavyo havigusi moja kwa moja maisha ya mwananchi wa nanjilinji.

Leo kumekuwepo na takwimu za kwenye makaratasi za kukua kwa uchumi wa nchi na hatimaye kuingia uchumi wa kati, uchumi huu wa kati unaendana vipi na uhalisia wa maisha ya wananchi wa kawaida? Au ni namna ya serikali kijipigia debe kuuonesha umma kuwa inafanya kazi yaani "inajitekenya na kucheka yenyewe". Uchumi huu wa kati unatakiwa uendane na maendeleo ya kijamii ikiwepo ajira kwa vijana na huduma mhimu za kijamii.

Ni ndani ya miaka mitano hii ambayo haki za binadamu zimeendelea kuvunjwa, watu wamepigwa risasi, wametekwa, kupotezwa, na wengine wameokotwa kwenye fukwe za bahari na kingo za mito wakiwa wamekufa. Ni katika awamu hii ambayo wote walioonekana kuwa na mlengo tofauti wa kisiasa eidha walifungwa kwa kubambikiziwa kesi za kichochezi ama waliwahishwa kuzimu. Yaani ajenda au kipaumbele cha serikali ya awamu hii ilikuwa kuua upinzani na kubaki na mlengo wa chama kimoja.

Ni ndani ya awamu ya tano ya serikali ya JMT ambapo bunge halikurushwa live, vyombo vya habari binafsi vilifungiwa pale viliporipoti habari ambazo hazikuwapendeza watawala, tumekuwa kwenye kipindi ambacho hautasikia chombo cha habari kikikosoa utendaji wa serikali, zaidi vyote vimegeuka kusifia ili kulinda mikate yao.

Ni miaka mitano ambayo tumeshuhudia uminywaji wa democrasia na Uhuru wa kujieleza, tumeshuhudia "AMRI TOKA JUU" ikifanya kazi kuliko hata mhimili wa mahakama na bunge. Viongozi wateule wa serikali walijawa na kiburi na kauli zilizoumiza wananchi.

Hivyo pamoja na mazuri machache ila mabaya haya mengi yanatosha kwa watanzania, makudindi yote, vijana, wazee, wafanyakazi wa umma na binfsi, walioko makazini na wasioko, wanaume kwa wanawake, pasipo kujali itikadi ya vyama vyetu, ni heri tufanye maamuzi sahihi ya kukomboa taifa, haki yetu ya kuheshimiwa tuirejeshe, Uhuru wetu wakujieleza uliopokwa tuurejeshe, tupate haki ya kuajiriwa na tufurahie matunda ya Tanzania yetu nzuri.

Watanzania kwa makundi yote, uwe CCM, Chadema, CUF, ACT-Wazalendo et al, tufanye kweli kuikomboa Tanzania yetu!
 
Kuna watu kuanza kufikiria vyema ndani ya miaka mitano serikali imefanya nini, hawawezi.

Kipimo kizuri ni kuangalia ndani ya hii miaka mitano mzunguko wa maisha ya mwananchi umekuwa mgumu au umekuwa na aheri kidogo,
Hapo watu hawawezi tambua.
 
Back
Top Bottom