Mwaka 2023 kulikuwa na Makosa 37,448 ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania, 15,301 yalikuwa kwa Watoto

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1724487938465.png

1724487966340.png

1724487977031.png
Soma Pia: Nini kinachangia ongezeko la matukio ya Ukatili dhidi ya Watoto?

Takwimu za Hall ya Uhalifu Januari - Desemba 2023.

Makosa ya Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto
Makosa haya ni yale yote yanayohusu ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto. Makosa haya yanatendeka zaidi katika jamii na hasa ndani ya familia, Jami imekuwa inakabiliana na changamoto zinazohusu makosa ya ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto kama vile kubaka, kulawiti, kutupa watoto, kutelekeza familia na ukeketaji.

Ukatili na unyanyasaji wa aina hii umekuwa ukiongezeka kila siku na jamii inashindwa kutetea watoto na kujiweka mbali na matatizo yanayowaathiri watoto. Kutokana na hali hii Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeendelea kuinua kiwango cha uelewa wa jamii na kuimarisha huduma ya Madawati ya Jinsia katika vituo vya polisi ili kuhamasisha wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2023 jumla ya Waathirika 15,301 wa ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto waliripotiwa ikilinganishwa na Waathirika 12,163 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

Hili ni ongezeko la Waathirika 3,138 sawa na asilimia 25.8. Waathirika wameripotiwa zaidi katika Mikoa ya Arusha (1,089), Mororgoro (976), Tanga (884), Kinondoni (789) na Mjini Magharibi (788).

Mikoa iliyokuwa na idadi ndogo ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia

Waathirika wa ukatili: na unyanyasaji wa kijinsia wameripotiwa zaidi katika Mikoa ya Kusi (100), Kusini Unguja (102), Kaskazini Pemba (103), Tarime Rorya na Kaskazini Unguja (161 kila mmoja). Makosa yenye idadi kubwa ya waathirika ni Kubaka (8,185), Kulawiti (2,382), Kumpa mimba mwanafunzi (1,437), Kumzorotesha mwanafunzi masomo (922) na shambulio la aibu (396).

Kutokana na hali hii, Jeshi la Polisi katika maboresho yake, limeunda Kikosi Kazi Maalum (kupitia Dawati la Jinsia) kwa ajili ya kufuatilia, kuratibu na kusimamia kwa karibu zaidi makosa dhidi ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.

Kwa kutumia kitengo hicho cha Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi limeendelea kuinua kiwango cha uelewa wa jamii na kuimarisha huduma ya madawati ya jinsia katika vituo vya Polisi ili kuhamasisha wananchi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Hatua hii imeleta mwitikio chanya katika kuripoti matukio hayo ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2023 jumla ya Waathirika 37,448 walifanyiwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ikilinganishwa na Waathirika 30,566 kipindi kama hicho cha mwaka 2022. Hili ni ongezeko la Waathirika 6,882 sawa na asilimia 22.5. Waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia wameripotiwa zaidi katika Mikoa ya Temeke (4,751), Arusha (4,565), Tanga (3,252), Kinondoni (3,150) na Hala (2,490).

Mikoa/Vikosi vyenye idadi ndogo ya waathirika ni Kusini Pemba (101), Kusini Unguja (105), Kaskazini Pemba (106), Tarime Rorya (161) na Kaskazini Unguja (175).

Makosa yenye idadi kubwa ya waathirika ni kubaka (8,691), shambulio (6,727), Shambulio la kudhuru mwili (5,497), kujeruhi (3,975) na lugha ya matusi (3,657), (Jedwali Na. 2.14).

TAKWIMU ZA UHALIFU TANZANIA DESEMBA 2023
 
Tuji tahidi kuwa Linda na kuwapa mazingira Safi watoto, maana mtaani Kuna majitu yana roho kavu sana
 
Noma sana . ila je, muamko wa wanajamii katika kuripot hayo matukio upo?

Mi naona kuna baadhi ya sehemu watu wanafumbia macho hayo matatizo hata kuripoti ili kupata ufumbuzi .
 
[emoji7][emoji7]
 
Back
Top Bottom