The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Hizi taarifa za serikali naona kama zinanipa maswali mengi bila majibu.
Mei 2024 aliekua waziri wa Utalii Angela Kairuki alisema kwa mwaka 2023 Tanzania ilipata watalii Milioni 1.8, ambayo ilikua ni ongezeko la 96% kulinganisha na watalii laki 9 wa mwaka 2021.
Januari mwaka huu, waziri wa Utalii Pimdi Chana aliyangaza kwamba mwaka 2024 Tanzania ilipata watalii milioni 5.4.
Shida yangu inakuja, Takwimu za mapato ya utalii kutoka benki kuu zinasema mwaka 2023 Tanzania iliingiza Dollar Bilioni 3.37 kutokana na utalii na mwaka 2024 Tanzania iliingiza Dollar Bilioni 3.67 kutokana na utalii.
Sasa tukirudi kwenye takwimu, ukiangalia 2024 kulikua na ongezeko la watalii karibu 3.6 milioni, sawa na ongezeko la 200% kutoka idadi ya watalii wa 2023 lakini mapato yameongezeka kwa kama 9% wakati idadi ya watalii imeongezeka kwa 200%.
Labda wataalamu mnisaidie kuelewa hizi takwimu zilivyokaa.
View: https://x.com/TanzaniaInsight/status/1890644239752786261?s=19

Loading…
habarileo.co.tz
Januari mwaka huu, waziri wa Utalii Pimdi Chana aliyangaza kwamba mwaka 2024 Tanzania ilipata watalii milioni 5.4.
Tanzania yavutia watalii milioni 5.36 mwaka 2024
swahili.cri.cn