Mwaka 2024 Kulikuwa na Pendekezo la Kuondoa Live Streaming ya Matokeo ya Urais: Je, Wewe Ulilionaje?

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Mwaka 2024, Seneti ilipokea Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi uliopendekeza kuondoa sharti la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuonyesha moja kwa moja (live streaming) matokeo ya uchaguzi wa urais.

​
Pendekezo hilo lilitaka matokeo yatumwe kwa njia ya kielektroniki kwa vituo vya kujumlishia kura, wagombea, mawakala na waangalizi wa uchaguzi ndani ya saa mbili baada ya kutangazwa katika vituo vya kupigia kura, badala ya wananchi kuyafuatilia mubashara kupitia mfumo wa live streaming.

Wakati huo, pendekezo hilo lilizua mjadala mkubwa nchini. Wapo waliodai lingeongeza ufanisi katika usimamizi wa uchaguzi, huku wengine wakisema kuondolewa kwa live streaming kungepunguza uwazi na imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi.

Kwa wengi wa wananchi, live streaming ilionekana kuwa njia muhimu ya kufuatilia matokeo kwa wakati halisi na kujiridhisha kuwa mchakato wa uchaguzi unaendeshwa kwa uwazi.

Je, wewe unakumbuka pendekezo hili la mwaka 2024? Unaamini live streaming ya matokeo ya uchaguzi inapaswa kuendelea au iondolewe? Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya maoni.
 
Ruto tayari anafuata nyayo za wenzeka akina sa100, m7 and pk.
 
Transparency haitakiwi.
Jk alifanya hivyo awamu yake ya mwisho baada ya kugalagazwa na Slaa baadhi ya mikoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…