Mwaka 2025, fanya dunia sehemu nzuri ya kuishi

Mwaka 2025, fanya dunia sehemu nzuri ya kuishi

maramojatu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
1,749
Reaction score
2,319
MwanaJF wenzangu,
Tunashukuru tumeanza wiki 1 ya mwaka 2025. Tuweke malengo ya kuhakikisha vizazi na vizazi vinaikuta sayari yetu salama.
Mimi nitafanya yafuatayo;

1. Kupanda angalau miti 5 ya matunda tofauti tofauti.

2. Kuendelea kutotumia vifungashio vya plastiki

3. Kwenda sokoni na mifuko na kapu langu (hii nimekuwa nikifanya muda mrefu).

4. Kuzima na kuwasha umeme muda unaotakiwa ili kupunguza upotevu.

5. Kutotumia vyakula na vitu vilivyopakiwa kwenye vifungashio kutoka nje ya nchi.

Wewe mwenzangu mipango Yako ni ipi ili dunia yetu iweze kuwa salama?
 
Back
Top Bottom