Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesisitiza kuwa mwaka 2025 ni mwaka wa mageuzi na wanawake hawatarudi nyuma katika mapambano ya kudai haki zao. Akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam, Semu ameeleza kuwa hali ya kisiasa nchini imezidi kuwa ngumu, huku wanawake wakiendelea kukumbwa na changamoto za kiuchumi, kijamii, na kisiasa.
Amesema licha ya matumaini yaliyokuwepo kwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wanawake bado wanakabiliwa na ukandamizaji, ukosefu wa huduma bora za afya, elimu, na ajira. Semu amewahimiza wanawake kuungana kudai tume huru ya uchaguzi, katiba mpya, na mageuzi ya kiuchumi yanayolenga ustawi wa wanawake na jamii kwa ujumla.
Akitaja ajenda za Wanawake 2025, amesisitiza kuwa ACT Wazalendo itaendelea kuwa bega kwa bega na wanawake katika kupigania haki zao. Amehitimisha kwa kuwataka wanawake wa Tanzania kuwa mstari wa mbele katika mageuzi ya kisiasa na kijamii, akisisitiza kuwa hakuna taifa linaloweza kukombolewa bila nguvu ya wanawake.
Soma, Pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025
Soma, Pia: Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atangaza nia ya kuwania Urais mwaka 2025