Mwaka 2025, nitakuwa Raia wa Marekani rasmi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Nina kitambulisho utaifa cha NIDA ambacho kitakachoisha mwaka 2025 ambapo automatic nakuwa sio mtu wa Taifa hili hadi ni-renew.

Kutokana na michakato kuwa mingi ya kupata kitambulisho NIDA sitakuwa na muda wa kutafuta kingine hivyo inabidi nirudishwe nchini kwetu, Marekani ili nisiendelee kukaa hapa kama mvamizi.

Wala msijali nimezaliwa wapi, kitambulisho cha utaifa kikiisha mimi nakuwa sio raia.

Niwatakie kila la kheri mtakao re-new kitambulisho. Endeleeni kukaa kwenye nchi ambayo umeme wake ni wa mgao+, maji ni shida. Kila mtu anakomba asali hadi watumishi wanasahaulika.

Kwa wale ambao hamta renew safari njema.
 
Hili jukwaa mbona linavamiwa na watu wa ovyo sana
 
Huo ndiyo ukweli japo umeponda. Hapa Tanzania kila kitu kukipata lazima uhangaike.
Kukipata kitambulisho cha NIDA ni muziki. Unafuatilia miezi 3 km hauna kazi ya kufanya
 
Nchi za kiafrika ni za kijinga sana. Tuna kila aina ya raslimali lkn bado tupo masikini.
George Wear ni raisi lkn mwanae ni raia wa Marekani. Shituka mkuu
Kama ni timoth weah yeye ni raia wa Liberia,Jamaica, Ufaransa na Marekani
 
Nina kitambulisho utaifa cha NIDA ambacho kitakachoisha mwaka 2025 ambapo automatic nakuwa sio mtu wa Taifa hili hadi ni-renew.

Kutokana na michakato kuwa mingi ya kupata kitambulisho NIDA sitakuwa na muda wa kutafuta kingine hivyo inabidi nirudishwe nchini kwetu, Marekani ili nisiendelee kukaa hapa kama mvamizi.

Wala msijali nimezaliwa wapi, kitambulisho cha utaifa kikiisha mimi nakuwa sio raia.

Niwatakie kila la kheri mtakao re-new kitambulisho. Endeleeni kukaa kwenye nchi ambayo umeme wake ni wa mgao+, maji ni shida. Kila mtu anakomba asali hadi watumishi wanasahaulika.

Kwa wale ambao hamta renew safari njema.
Umechafukwa! Nchi ya hovyo Sana hii! Watu wanalamba asali tu!
 
Back
Top Bottom