molasses ni mabaki ya miwa, yani katika uchakataji wa kuzalisha sukari. Mabaki hayo yanakuwa kwenye mfumo wa kimiminika mithiri ya asali. Molasses utumika kutegea mtego wa kuwakamata hao vipepeo wajulikanao kwa jina la nondo. Mtego huo utengenezwa kwa kutumia dumu la njano lenye ujazo wa lita tano, dumu hilo linatakiwa kukatwa ubavuni pande zote mbili kuanzia chini kwenda juu. Kila ubavu litakatwa pande zote mbili kwa kuanzia chini utakata juu kidogo kama sentimita nne kutoka chini kwenda juu mpaka kwenye mshazari wa dumu lilipoanza kuingia ndani. Kisha molasses itajazwa ndani ya dumu na kuninginizwa shambani kwa kutumia mti uliyopigiliwa ardhini. Dumu la rangi ya njano linatumika kwasababu ile rangi yake inawavutia nondo. Hivyo basi nondo akivutiwa na ile rangi atapaa mpaka kwenye dumu lile, na baada ya kutua pale ile halufu ya molasses itamvutia kuingia ndani ya dumu kupitia pande za dumu zilizokatwa. Akishatua ndani ya dumu ile molasses ipo kama gundi itamnasa hivyo hataweza kutoka tena, yani vuta picha kipepeo atue kwenye asali lazima atanasa hataweza kuruka kutoka hapo. Lengo la hili zoezi ni kuzuia hawa nondo wasitage mayai kwa wingi kwani anaponasa kwenye mtego hataweza kutoka hapa na mwisho wa siku atakufa hapo hapo. Katika hatua za ukuwaji wa mdudu nondo upitia hatua nne yani mayai-funza-pupa-nondo mwenyewe(adults) na hatua hatarishi katika ukuwaji wake ni hatua ya funza (larva stage) ambayo ndiyo hujulikana kama kiwavi jeshi. Hivyo mtego usaidia kuzibiti hii changamoto.