The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Mwaka huu kama umegombea kwenye kura za maoni, ukashinda halafu kamati kuu au wenye chama wakakata jina lako huna mbadala kama iliyokuwepo siku za nyuma, kwamba utakimbilia upinzani ugombee.
Kama mnavyosikia, alisema Polepole na jana pia amesema Waziri Mkuu kuwa kura za maoni hazikua na maana yoyote, maamuzi yote yako kamati kuu, wao ndio watarudisha jina la Mgombea hata kama ukiwa wa mwisho na kura 0 bado unaweza kurudishwa kua mgombea. Na akamhakikishia shehe majini kua atakua mgombea kule Handeni.
Kinachofanyika mwaka huu, kamati kuu ya CCM itapeleka majina ya Wagombea wa majimbo yote Tume ya Uchaguzi kimia kimia. Ikishafika siku ya mwisho ya kurudisha form ya kuomba kuteuliwa na Tume kwa vyama vya siasa basi Tume itatangaza majina ya wagombea wote hivyo kama ulikatwa unakua huna nafasi ya kuhamia chama kingine kwa sababu muda unakua umeshapita.
CCM wanahofia kua wakitoa majina mapema wale ambao hawatakubaliana na maamuzi ya kamati kuu ya chama au maamuzi ya wenye chama basi wanaweza kukimbilia upinzani na hatimae wakapata nafasi ya kugombea na kushinda uchaguzi.
Hivyo kama uligombea kwenye kura za maoni ukawa mshindi kwa kura nyingi, wenye chama wasipokutaka huna mahala pa kukimbilia. Hivyo wagombea wote jiandaeni na matokeo yoyote yatakayokuja.