Uchaguzi 2020 Mwaka huu kama umegombea CCM, ukikatwa jina lako huna mbadala, majina yote kutolewa siku ya mwisho na NEC


Mla na mtoa rushwa anatakiwa kufikishwa mahakamani, na sio kwenye hizo kamati za siasa chafu. Huko kwenye hizi kamati ni kichaka kingine cha kulia rushwa, na kupitisha watu kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani huko ccm.
 
Huko ccm nani ambae hatoi rushwa?!
CCM ni Muungano wa Katiba, kanuni, sheria na taratibu na miongozo mbalimbali, bila kusahau wanachama na viongozi. Hivyo basi kwa kuwa wanachama na viongozi ni watu na kwamba tabia ya kupenda na ya kuchukia rushwa ni tabia za watu. Na kwa sababu hiyo, CCM imetamka wazi kuwa sifa ya kiongozi anayetokana na CCM, ni lazima awe mtu ambaye tabia yake ni ya kuchukia rushwa.

Na ndio maana ndani ya CCM zipo idara mbalimbali ikiwa ni idara ya maadili, ambayo ndiyo inayofuatilia kwa ukaribu tabia na miendendo ya wanachama. Mwanachama awaye yote akifahamika na ikathibitika ni mwenye tabia ya kupenda rushwa, hafai kuwa kiongozi katika nafasi yo yote ile ndani ya chama au serikalini.
 
QUOTE="tindo, post: 36202739, member: 55693"]
Mla na mtoa rushwa anatakiwa kufikishwa mahakamani, na sio kwenye hizo kamati za siasa chafu. Huko kwenye hizi kamati ni kichaka kingine cha kulia rushwa, na kupitisha watu kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani huko ccm.
[/QUOTE]
Wewe umesema. Na bila shaka umehisi tu. Sifikiri kama umewahi kuwa mwana kamati hizo ambazo umezisemea.
 
Mla na mtoa rushwa anatakiwa kufikishwa mahakamani, na sio kwenye hizo kamati za siasa chafu. Huko kwenye hizi kamati ni kichaka kingine cha kulia rushwa, na kupitisha watu kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani huko ccm.

Wewe umesema. Na bila shaka umehisi tu. Sifikirii kama umewahi kuwa mwana kamati hizo ambazo umezisemea.
 
Wazee wa kusubiri makombo wanatamani kulia!!! Tuliwaambia hawa jamaa wanawezaje kuchukua nchi wakati hata wagombea hawana????

Queen Esther
 
Mleta maada atakuwa na shida kubwa sana. Waziri mkuu alisema anamwombea huyo Shehe majini apitishwe na kikao cha kamati. Ajabu kama mwendawazimu, mleta maada anakuja kusema "waziri mkuu kamhakikishia". Watu kama hawa ndio hufanya media outlets kufungiwa au kuchukiwa na serikali.
 
Majimbo ambayo mshindi katofautiana pakubwa na anayemfuata wamtangaze tu hata leo kuwa mgombea eg Makamba,Tulia maana hao wenye 0&1 sioni kama wana athari hata wakim-support wa upinzani.

Majimbo kama Chalinze wakikurupuka wanaweka jimbo rehani.

Machaguo ya wajumbe yangeheshimiwa tu labda pawepo sababu ya msingi sana.

Mtu anaweza akahamia upinzani dakika za mwisho si kwa ajili ya kugombea bali kugawa kura.
 
Hujui ulichoandika mkuu
 
What if Kama nina mtu pale NEC akanimegea za chini ya kapeti?

Utakosa moral legitimacy kwa wananchi, tofauti na kwamba ulishinda kwenye kura za maoni then ndipo ukakatwa! Kwahiyo, CCM watakapokunanga kwa wananchi huwezi kuwa na hoja nzito za kujitetea
 
Safi sana hii,kupunguza malaya wa kisiasa
 
Hiyo hiwezekani màana wagombea wanatakiwa wachukue from na kuzirejesha zikiwa zimejazwaikamilifu ndipo wateuliwe na tume
Hiyo ni rahisi Sana..aliyeteuliwa anapewa form same day na kuirejesha.. sidhani kama unahitaji zaidi ya 2hours kujaza form..but huwezi kuhamia chama kipya,ukapewa Kadi,ukateuliwa kugombea,ukachukua form NEC na kujaza same day.. hiyo ikitokea basi tegemea fujo na makundi kwenye chama husika.
 
Wakifanya hivyo ni kudhihirisha uoga usio na kifani. Watajidharaulisha sana.
 
wakifanya hivyo ccm nawambia mteenda kutengeneza ya tukose wote kwenye majimbo ushauri wa bure nawapa tu washindi watangazeni tu then tafuta dawa ya mwarobain kuelekea 2025 mkiwa kama chama dola ua chama pinzani ,wenda mawazo yenu ni mazuri kutokana na tuyasikiayo kutoka katika majimbo huko ila si mda muafaka wakufanya hicho kwa sasa vinginevyo mwafa kabisa kabla ya saa mbili hasubui nawambia ccm punguza kujiamini sana mwaka huu hauko vizuri kwenu huo ndo ukweli uzuri tunao yasema haya hatuna vyama but ni wapenzi wa democracy
 
Hivi unaujua utaratibu au unaandika kwa kufuata matamanio yako?
Mgombea Ni lazima apewe fomu na NEC bàda ya kupewa barua ya uteuzi na chama chake,kwa maoni yako chama kikipeleka majina kinyemela hizo fomu watapewaje
 
Umeanza vizuri una Kuja Kuvurunda mwisho
Eti ccm inaogopa iogope nini
Ccm inaweza ogopa kivuli chake kweli
Kama kweli ccm majasiri, iweje mnazuia wapinzani wasifanye mikutano yao ? Enzi ya kikwete mliona ule mziki, maandamano na mikutano, opresheni sangara nk., Magu tumbo moto. Pia ccm wamepora uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana. Woga wa nini, kama mnatekeleza ilani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…