Pre GE2025 Mwaka huu wa uchaguzi umepoa sana hakuna zile amsha amsha kama za 2015

Pre GE2025 Mwaka huu wa uchaguzi umepoa sana hakuna zile amsha amsha kama za 2015

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
790
Reaction score
1,373
Mwaka wa uchaguzi ndio huoo, lakini umepooa kama uji wa mgonjwa? Hakuna zile amsha amsha tulizo zizowea kama kipindi kile cha mwaka 2015 ambapo vijana wa 4u Movement waliungana na vijana wa M4C kumsimamisha na kumpigania mzee Lowahasa (wakamsifu na kusema nywele nyeupe na roho nyeupe, kashafa ya Richmond alisingiziwa na mwenye hiyo kampuni ni bwana mkubwa!).

Unaambiwa kipindi kile ilikuwa mwache mwache hatumwi mtoto dukani, CCM wenyewe walilianzisha wakaimba tunaimani na Lowasa alivyo katwa jina lake, ikapelekea makada kindakindaki kama Dk. Nchimbi na Sofia Simba kupewa adhabu kali! Vyama vya upinzani vikaungana kutengeneza UKAWA kule Lipumba anauwasha moto, huku Mbatia anakomelea sindano kule dokta Makaidi wa NLD bila kusahau Maalim Seif kule Zanzibar na Dkt. Slaa, ikapelekea wazee wa kaunda suti kucheza figisu kali na kumwaga mpunga kwa Dkt Slaa na Lipumba wakasaliti vita hata kabla ya mapambano na kukimbilia ughaibuni, makamanda wakawaambia aluta continua mapambano yanaendelea.

Kila siku macho kwenye TV magazeti yanauzwa kama njugu, kule Uhuru pale Tanzania Daima kule Mwananchi watu wanafanya biashara. Ilibidi idara zote ziingie kazini kumpigania anko Magu (alale anapo stahili) kumnadi kwa lazima Jahkaya na mzee wa Lupaso hawakuwa nyuma kumtetea anko Magu aliyekuwa hauziki mbele ya Lowahasa....., mpaka mzee wa Lupaso akaita watu wapumbavu pale Dodoma walipokuwa wakifunga kampeni zao watu wakabaki midomo wazi.

Hakuna mwaka upinzani ulileta amsha amsha kama mwaka ule wa 2015 ilipelekea mpaka Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kule Z'bar na huku bara upinzani kususia matokeo na kukataa kumtambua raisi mteule!

Kwa sasa naweza kusema kwamba CHADEMA imeshindwa kucheza karata zake vizuri wamesahau kwamba ndicho chama mbadala cha upinzani kilichobakia, matokeo yake kila kukicha ni kuvuana nguo na kutukanana hadharani. Nilitegemea adui yao namba moja awe ni CCM iweje wapopoane mawe wao kwa wao?

Yote tisa kumi, lamgambo limeshalia huko Dodoma kada wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi amesha tangazwa ashirikiane na mama wa Kizimkazi kupeperusha bendera ya chama vipi kwenu CHADEMA mbona kimya? Macho yote yamebaki kwenye uchaguzi wa kumsaka mwenyekiti na endapo Mbowe ama Lisu atashinda kwenye kiti hicho kambi itakayo bakia itakuwa imepasuliwa vipande vipande. Mtawezaje kuungana tena kupigana na hili lidude likubwa CCM ambalo limejichimbia mizizi katika kila idara ya kitaifa?

Hapa nawaonya CHADEMA msithubutu kumsimamisha Lisu ama Mbowe kwenye kiti cha uraisi katika uchaguzi huu wa 2025 kwani itakuwa ni jambo rahisi sana kwa mama Kizimkazi kuwapasua pasua vipande vipande. Tafuteni mtu asiye na makundi msomi na aliye mpya kwenye macho na masikio ya watu ili aweze kuleta tumaini jipya, ama la mtabaki kuwa wasindikizaji kwenye uchaguzi huu, mtawapa kazi ndogo sana kamati ya kampeni ya CCM.
 
Back
Top Bottom