The Mongolian Savage
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 8,082
- 17,838
Yeereeeeeh!
Wadau mnaendeleaje!
Huyu mwamba mchungaji ni wa kipekee.
Kanisa lake simple tu la mabati huko Meru milimani enzi hizo.
Kuukaribisha mwaka mpya 2007 mwamba alitupanga nakutuambia shida zote mtaziacha nyuma 2006 na mwaka wa 2007 nawaakikishia njia zenu zote Yesu atazifagia hamna kujikwaa tena. Na kweli alisema ukweli.
Tulikuwa kundi Dogo tu kama la waumini wasiozidi 15. Wakati huo nilikuwa kachalii tu sana.
Saa nne usiku desemba 31 2006 tukajumuika ndani ya kanisa. Mchungaji akatuonya hakuna kutoka nje kusheherekea mwaka mpya ni kufanya maombi ndani na maombi yenyewe kulitaja jina la YESU tu mfululizo.
Ilipofika saa tano na nusu. Mchungaji akatuambia tutataja jina la Yesu mfululizo hadi saa saba usiku na kutaja matamanio yetu yote kimoyomoyo. Mimi maombi yangu yalikuwa Yesu anisaidie niende mamtoni.
Basi tukaanza kulitaja jina la Yesu mdogomdogoYESU YESU YESU YESU YESU ila ilibidi tumalize saa sita na nusu badala ya saa 7kwasababu polisi kwenye difenda walishaanza kufyatua risasi juu kutawanyisha watu warudi makwao
Ilipogonga tu saa sita kamili na kelele nyingi huko nje wakishangilia mwaka mpya sisi huku ndani tukazidi kupaza sauti za Yesu mfululizo YESU YESU YESU YESU YESU huku tukirukaruka na kushangilia hadi saa sita na nusu.
Mwaka huo wa 2007 ulininyookea vibaya sana hadi leo najikuta mamtoni.
Yesu alinitoa kwa kumtumainia.