Mwaka unakaribia kuisha nimepata mualiko moja tu wa harusi, hali kwenu ipoje?

Mwaka unakaribia kuisha nimepata mualiko moja tu wa harusi, hali kwenu ipoje?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Mwaka unaisha hivyo ni harusi moja pekee niliyoalikwa, ni tofauti na miaka ya nyuma.

Labda pengine mlolongo wa matukio kadhaa umefanya mwaka huu kutokuwa kwenye mipango ya kuoa kwa vijana mabachela naowajua, maana kama ni michango ipo.

Pengine nikadhani labda tatizo ni uchumi ila nimekataa kwasababu kazini kuna vijana mabachela na wana uwezo mpaka wa kugharamia harusi, ni jambo la kusikitisha

hali kwenu vipi
 
Mwaka unaisha hivyo ni harusi moja pekee niliyoalikwa, ni tofauti na miaka ya nyuma.

hali kwenu vipi
Tangu 2022 kiwango na idadi ya ndoa kimeendelea kushuka kwa kasi sana , na kuelekea mbele tuendako, idadi inaweza kushuka zaidi na hatimae habari za kufunga ndoa zitatokomea kabisa.

Mshukuru Mungu kualikwa kwenye ndoa ambayo hujachangia 🐒
 
Back
Top Bottom