Mwaka wa gari una uhusiano na toleo la gari?

Mwaka wa gari una uhusiano na toleo la gari?

starspoint21

Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
33
Reaction score
12
Habari wa JF.
Heri ya mwaka mpya.

Kuuliza sio ujinga wakuu tena kwenu wana JF heshima kwenu. Kwa wale wajuzi wa magari na wafuatiliaji wa magari ningepanda kufahamu wanaposema hii gari ni ya mwaka 2007 au 2012. Wanamaanisha hilo gari limetengenezwa mwaka huo au ni toleo la mwaka huo tajwa?
 
Na Wanaposema ni namba D, A,.C inamaanisha nn?

Namba Za Usajili, Za zamani kabisa zinaanza na A wakati mpya kabiza zinaanza na D mpaka sasa hv ila D zikiisha zitaanza tena E

Kwahiyo ikianza na kwamfano T 859 AYD ujue haya magari yapo toka enzi za mwalimu nchini
 
Shukrani mkuu. So ina maana mwaka huu ukinunu gari la mwaka 2007 ni kwamba umenunu gari ambalo lina miaka 11.[emoji22]

Exactly lakini kama utaagiza ni kwamba halijatumika nchini, ila limetumika huko kwa wenzetu
 
Namba Za Usajili, Za zamani kabisa zinaanza na A wakati mpya kabiza zinaanza na D mpaka sasa hv ila D zikiisha zitaanza tena E

Kwahiyo ikianza na kwamfano T 859 AYD ujue haya magari yapo toka enzi za mwalimu nchini
Umeelezea vizuri sana mkuu natumaini Ziltan atakuwa ameelewa.
 
Shukrani mkuu. So ina maana mwaka huu ukinunu gari la mwaka 2007 ni kwamba umenunu gari ambalo lina miaka 11.[emoji22]
Tena utasikia mbongo anakuambia ameagiza gari mpya tena new model...magari mengi tunayoyaona barabarani ni mitumba iliyochokwa na wajapani
 
Namba Za Usajili, Za zamani kabisa zinaanza na A wakati mpya kabiza zinaanza na D mpaka sasa hv ila D zikiisha zitaanza tena E

Kwahiyo ikianza na kwamfano T 859 AYD ujue haya magari yapo toka enzi za mwalimu nchini
Kwa kuongezea.

Mfano magari ya serikali, SM, ST n.k. lililokua nchini tangu mwaka 1970, leo akilinunua mtu binafsi atatakiwa kulisajili hivyo atapewa namba D.

Kwahiyo unaweza kukuta Toyota Hilux ina namba T 100 DKN kumbe lipo nchini tangu enzi za mwalimu
 
Back
Top Bottom