Elections 2010 Mwakala Chadema wapewe SIM card mbili usiku wa kuhesabu kura

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Wadau, wapenda haki:

Kuna taarifa kwamba kuna baadhi ya mitandao ya simu za mkononi zitafungwa kuanzia jioni siku ile ya kupiga kura (wakati wa kuhesabu kura) ili kusiwepo mawasiliano kati ya mawakala wa vituo na viongozi wa vyama mbali mbali.

Ili kuhakikishe mawakala na viongozi wa chama tawala CCM wanawasiliana, basi wao watapewa SIM card ya ile/ule mtandao ambao mafisadi hawana uwezo nao.

Nakiri mimi nashindwa kuamini habari hii, lakini lolote lawezekana kwa hawa CCM kwani kumnyan'ganya mtu mnofu ulio mdomoni si kitu anachoweza kuridhia kiurahisi. Viongozi wa Chadema wawe macho kuhusu hili -- na ikiwezekana mawakala wao wawe na simu zenye mitandao angalau miwili to be on the safe side.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…