Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,437
- 4,618
Fidelis butahe, Iringa
ALIYEKUWA mshindi katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fredrick Mwakalebela jana alikuwa kivutio na kufunika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Jakaya Kikwete baada ya kutakiwa kupanda jukwaani.
Katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Samora mjini hapa, wananchi walililipuka kwa shangwe na vigeregere huku wakimtaja jina lake mpaka mgombea huyo alipopanda jukwaani.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwakalebela aliwaomba wanachama wa CCM wa Iringa Mjini kuvunja makundi, kwani anaamini kuwa bado chama hicho kina nafasi.
"Wana Iringa kila kitu tunachokiona hapa kimeletwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wabunge na madiwani wa CCM. Napenda kuchua fursa hii kuhakikisha chama chetu kinashinda Iringa..."
"Napenda kusema mbele ya Rais Jakaya Kikwete tukiunge mkono chama chetu, kwani tulikuwa watu 12, lakini sasa tuwe kundi moja. Natangaza kuvunja makundi, wapinzani wasitutumie kama mtaji," alisema Mwakalebela huku wananchi wakishangilia na kelele za sauti ya juu.
Baada ya kumaliza kuzungumza na kushuka jukwaani, Mwakalebela alikumbatiana na Kikwete na kisha kushikwa mkono na mgombea huyo wa urais hadi jukwaani tena na kuonyeshwa kwa wananchi.
"Mmemuona Mwakalebela?" alihoji Kikwete mbele ya umati wa wananchi waliofurika katika mkutano huo, wananchi walijibu 'tumemuona" huku wakiendelea kushangilia na kumkumbatia tena Mwakalebela akiwa naye jukwaani.
Kabla ya Mwakalebela kuzungumza Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Deo Sanga 'Jah peaple' aliwaita wagombea wanne waliokuwa katika kinyanganyiro cha kura za maoni ambapo kwa nyakati tofauti walieleza kuvunja kambi zao na kuumuunga mkono mgombea alisimamishwa kwa tiketi ya chama hicho, Monica Mbega.
Awali, mgombea ubunge katika jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega, aliwaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM, kwani chama hicho kimeweza kutekeleza sehemu kubwa ya ahadi walizozitoa miaka mitano iliyopita.
Mgombea huyo alipoitwa jukwaani na Kikwete hakushangiliwa kama ilivyokuwa kwa Mwakalebela na hata alipoanza kuzungumza baadhi ya watu katika uwanja huo walianza kuondoka.
Mwakalebela ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alishinda nafasi ya kugombea ubunge Iringa Mjini kwa kupata kura 3,897 dhidi ya Mbunge aliyepita, Monica Mbega aliyepata kura 2,989 katika matokeo ya kura za maoni CCM.
Mwakalebela alitumia dakika tatu kuzungumza na wananchi waliofurika katika uwanja huo huku sauti yake ikisikika kwa shida kutokana na shangwe na kelele kutoka kwa wananchi hao.
Akizungumza na wananchi uwanjani hao Kikwete alisema hospitali ya mkoa huo itaboreshwa pamoja na kujenga maabara.
"Hospitali ya mkoa iendelee kuwa ya mkoa, ya wilaya itajengwa na kuongezwa kwa vituo vya afya ili watu wasijazane katika hospitali hizi" alisema Kikwete.
Akijinadi kutetea kiti chake katika Jimbo la Kalenga, Rais Kikwete aliwataka wanawake nchini kutokuwa na hofu na kwamba katika serikali ijayo ya miaka mitano itaendelea kuwapa kipaumbele katika nafasi za uongozi mbalimbali
SOURCE: MWANANCH