Mwakaleli (kijiji cha Kandete) bei za mashamba zipoje ili nisipigwe?

Mwakaleli (kijiji cha Kandete) bei za mashamba zipoje ili nisipigwe?

Root root AE

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
207
Reaction score
354
Habari wakuu?

Kwa atakayekua amesoma uzi wangu wa unaouliza sehemu nzuri ya kuishi kati ya Tukuyu na Kyela atakua anajua.

Kikubwa ni kwamba sehemu niliyochagua kuishi ni Tukuyu eneo la Mwakaleli kijiji cha Kandete. Ninataka nikifika ninunue shamba dogo kwaajili ya chakula (ndizi, viazi Ulaya, mboga mboga nk) na sio kwa ajili ya kujenga. Hivo naomba msaada wa kujua bei za kununua mashamba au hata kama ni kwa kukodisha zipoje?

Sitaki shamba kubwa sana, hata nusu/robo hekali itanitosha kabisaa.
 
Hakuna mashamba makubwa kwa kuwa maeneo mengi ni mashamba ya chai na miti. Pia wakazi wengi hugawana mashamba madogo madogo (imbaka au utupaka) kiukoo au kifamilia. Ni kama ilivyo uchagani, huwezi kupata shamba kirahisi. Ekari moja haiwezi kupatikana kwa mtu mmoja labda uunganishe watu wawili au watatu. Na Kandete ni mjini, si mashambani!

Binafsi nina shamba kijiji cha jirani Lugombo linakaribia ekari moja, nauza milioni 3. Kuna maji ya bomba, umeme wa REA hapohapo shambani na barabara. Maeneo hayo hulimwa sana maparachichi na hustawi sana hata kaeneo kadogo. Pia viazi mviringo huzaa sana!

Karibu sana Mwakaleli, bonde la neema, hali ya hewa safi, watu wakarimu na wacha Mungu.
 
Naona umekandia upande mmoja ili uupigie debe upande wako ila sio mbaya vp kutoka Kandete mpaka Lugombo ni km ngapi/muda gani?
 
Hakuna mashamba makubwa kwa kuwa maeneo mengi ni mashamba ya chai na miti. Pia wakazi wengi hugawana mashamba madogo madogo (imbaka au utupaka) kiukoo au kifamilia. Ni kama ilivyo uchagani, huwezi kupata shamba kirahisi. Ekari moja haiwezi kupatikana kwa mtu mmoja labda uunganishe watu wawili au watatu. Na Kandete ni mjini, si mashambani!

Binafsi nina shamba kijiji cha jirani Lugombo linakaribia ekari moja, nauza milioni 3. Kuna maji ya bomba, umeme wa REA hapohapo shambani na barabara. Maeneo hayo hulimwa sana maparachichi na hustawi sana hata kaeneo kadogo. Pia viazi mviringo huzaa sana!

Karibu sana Mwakaleli, bonde la neema, hali ya hewa safi, watu wakarimu na wacha Mungu
Ndaga kikolo,unauzavkwa nini kikolo!?Si upande maparachichi?
 
Nenda ukathibitishe. Kama wewe ni mwelewa, kwenye miji hakuna mashamba bali kuna viwanja! Kandete is now a town centre na lami ipo. Nimetoa mfano wa uchagani, uliza kama kuna kijiji cha kupata hata nusu ekari.

Kandete mjini hadi Lugombo ni takribani km 1. Kwa pikipiki ni dk 10-15, kwa mguu ni nusu saa ukipita mkato. Mwakaleli yote ni kwetu, hivi sasa sina ambapo ni kwangu japo ni asili yangu na nimeishi vijiji vyote 6 vya kata ya Kandete. Isange ni kata nyingine, kaulizie. Kwa sasa naishi mkoani Rukwa
Naona umekandia upande mmoja ili uupigie debe upande wako ila sio mbaya vp kutoka Kandete mpaka Lugombo ni km ngapi/muda gani?
 
Nenda ukathibitishe. Kama wewe ni mwelewa, kwenye miji hakuna mashamba bali kuna viwanja! Kandete is now a town centre na lami ipo. Nimetoa mfano wa uchagani, uliza kama kuna kijiji cha kupata hata nusu ekari.

Kandete mjini hadi Lugombo ni takribani km 1. Kwa pikipiki ni dk 10-15, kwa mguu ni nusu saa ukipita mkato. Mwakaleli yote ni kwetu, hivi sasa sina ambapo ni kwangu japo ni asili yangu na ni nimeishi vijiji vy
Unafikiri kwanini mahakamani wanahitaji ushahidi...kwasababu kikubwa sio uelewa bali ni uthibitisho na ndo nnachokitafuta mkuu sio vinginevyo
 
Isange nako kuzuri sana. Mandhari yake inapendeza mno hasa ukitazama safu za milima ya ukinga (Livingstone). Ila ni maeneo yaliyojaa makazi ya watu, hakuna mapori.

Nilizaliwa Tukuyu lakini nikalelewa na kukulia Mwakaleli. 2015 niligombea ubunge wa jimbo la Busokelo kupitia ACT-Wazalendo, nikagaragazwa vibaya na Mwakibete!
Kandete, isange
 
Isange nako kuzuri sana. Mandhari yake inapendeza mno hasa ukitazama safu za milima ya ujinga (Livingstone). Ila ni maeneo yaliyojaa makazi ya watu, hakuna mapori.

Nilizaliwa Tukuyu lakini nikalelewa na kukulia Mwakaleli. 2015 niligombea ubunge wa jimbo la Busokelo kupitia ACT-Wazalendo, nikagaragazwa vibaya na Mwakibete!
🤣🤣🤣🤣 pole sana mkuu....sehemu ambazo hazijajaa makazi ya watu ni wapi? me ndo nakutaka huko...
 
Sawa kabisa. Kyejo yote nimetembea na Lusanje ni kijiji kizuri sana hasa ukiwa maeneo ya mlimani Kyejo, unaliona bonde lote la Mwakaleli linavyopendeza. Isingekuwa kubanana sana, hakika nisingetoka nyumbani. Kukaja kununu mwe!

Mara nyingi huwa nakuja Dodoma kuwaandikia miradi ya maendeleo wabunge. Pamo atukwisa kwaghanila linga Kyala atupeele ubwumi.
Tununu,mimi nipo Dodoma,Mwakaleli nimekaa sana kwa babu na bibi Lusanje karibu na secondary ya kyejo,Ni kweli Kandete ni mji labda aende mbali,Luteba,Matamba nk.
 
Back
Top Bottom