Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Ujenzi, Archtect Elius Mwakalinga leo amehitimisha safari ya kuomba kura kwa Wajumbe wa Kata mbalimbali ndani ya Jimbo la Kyela Mkoani Mbeya anakotarajia kugombea Ubunge endapo atapata ridhaa ya wajumbe kumpitisha.
Zoezi hilo lilianza baada ya majina yao kutangazwa July 29 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla Jijini Dodoma.