Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
VILIO na simanzi jana vilitanda katika viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa Msanifu kurasa wa za magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communicatons Ltd (MCL), Adam Mwakibinga, aliyefariki juzi, baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi.
Huzuni walizokuwa nazo watoto wa marehemu, Lawarid na Farid, zilisababisha mamia ya watu waliohudhuria msiba huo, kububujikwa na machozi hasa pale waliposikika wakisema
Tutamtoa wapi baba mwingine."
Mwakibinga ambaye mwili wake ulisafirishwa kwenda Dodoma, anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Makuburu, mjini humo.
Akizungumza katika msiba huo, shemeji wa marehemu, Bebe Ndoje alisema Mwakibinga alifariki juzi saa 10.00 jioni na kuwa taratibu za mazishi zimekamilika.
Wakielezea hisia zao, baadhi ya Wafanyakazi wa MCL walimwelezea Mwakibinga kuwa alikuwa mchapa kazi, mcheshi, mkarimu na kwamba kifo chake kimeacha pengo kubwa.
Msanifu wa kurasa wa MCL, Ally Mkoreha alisema kwa kipindi cha miaka miwili alichofanya naye kazi Mwakibinga kwa karibu, alijifunza mengi kutoka kwa marehemu.
Mkoreha alisema pamoja na sifa nyingine, marehemu alikuwa mcheshi na asitekuwa na majivuno.
"Nimefadhaika na kuumia sana, Mwakibinga alikuwa rafiki yangu na nilikuwa naye kwenye dawati hili, sina la kusema kwani sijui kama pengo hili litazibika,tunachopaswa kukifanya sote ni kumuombea dua ili Mwenyezi Mungu umweke mahali pema peponi," alisema.
Mwakibinga ambaye ameacha mke na watoto wawili, alizaliwa mwaka 1974 mjini Dodoma na alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Mwenge, mkoani Tabora, kabla ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1985.
Mwaka 1988,alihitimu kidato cha sita na kisha kujiunga na mafunzo ya uandishi wa habari ngazi ya cheti.
Katika uhai wake, Mwakibinga aliwahi kufanya kazi mbali mbali ambapo Mwaka 1985 alifanya kazi ya Ukarani wa Mapato katika Mamlaka ya Maji Dodoma na baadaye. akajiunga na gazeti la Dar leo kama msanifu.
Mwaka 2005 hadi 2006 alikuwa Mwakilishi wa Kampuni ya Business Times, wilayani Rungwe, kabla ya Kujiunga na MCL.Mungu ailaze Roho la Marehemu Mahali pema Peponi.
Chanzo Mwakibinga kuzikwa Dodoma leo
Mwakibinga Mwenyeezi Mungu amlaze Pema Peponi Ameen.