HarakatiNews
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 218
- 187
Mwakilishi kutoka shirikisho la soka Duniani (FIFA) amekagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandi katika uwanja wa mpira wa Kaitaba na kuomba kasi ili ukamilke ka muda uliopangwa.
Mwakilishi huyo wa FIFA Mhandisi Kelvin Macklain, ametua bukoba na kukagua hatua kwa hatua uwanja huo,na alifika hapo kukagua hatua za mwisho kabla ya nyansi husika kuanza kutandazwa, na tayari zipo katika uwanja huo.
Akiongea na kituo hiki uwanjani hapo Mwakilishi huyo wa FIFA, amesema ni utaratibu wa FIFA kujilidisha na kazi ya maandalizi ya awali kabla ya kuruhusu nyasi bandia kutandazwa ,katika viwanja wanavyojenga wao duniani kote, huku Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja huo Pierre De Groote akisema watamaliza kazi yote mwezi Disemba mwaka huu.
Hata hivyo Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba Malick Tibabimale, amesema kuwa sehemu ya kati ya uwanja itakamilika ndani ya mwezi mmoja, na timu ya Kagera sugar itaanza kutumia uwanja huo baada ya mechi zake nne za mzunguko wa kwanza, itakapotumia uwanja wa musoma kama uwanja wake wa nyumbani katika ligi kuu ya vodacom itakayoanza kutimua vumbi septemba 12,2015.
[TD="align: center"]
[/TD]
[TD="align: center"] Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja wa Kaitaba Pierre De Groote akiongea na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya uwanja huo,nyuma yake ni katibu wa chama cha Soka Bukoba Malick Tibabimale
[/TD]
Chanzo: SomaHabari