magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 11,075
- 24,634
BONDIA Hassan Mwakinyo amepanda hadi nafasi ya 43 kwenye viwango vya ngumi vya dunia. Bondia huyo namba moja nchini ametajwa kuwa bondia wa nyota tatu duniani ,akihitaji kutafuta nyota nyingine mbili ilikuingia anga za mabondia wanaotambaduniani akiwamo Manny Pacquiao mwenye nyota tano.
Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia saa chache zilizopita leo Jumatano Novemba 25, 2020, Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 43 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa superwelter.
Mwakinyo aliyewahi kuwa bondia namba14 wa dunia baada ya kumchapa Sam Eggington nchini Uingereza mwaka 2018 aliporomoka mwaka jana hadi nafasi ya Bondia huyo licha ya kushinda mapambano kadhaa mwaka huu likiwamo la Tshibang Kayembe, alibaki nafasi ya 78 mpaka leo vilipotajwa viwango vipya na kupanda hanafasi ya 43.
Chanzo : Mwanaspoti.