Mwakinyo ashinda pambano lake dhidi ya Tinampay

Hahahaha, Jana nilimkataa huyo jamaa, kama kashinda sawa hongera zake, ila uzalendo wa hoya hoya nao mgumu?
Hahah we kua tu mpole mzee baba,maana hata jana Magu alishukuriwa kwa kua tangu ameingia ofisini na sisi tumepata kuonekana kwny Ngumi za kimataifa.

Uzalendo mbele mkuu.
 
Naombeni kujua UTIMAMU WA AKILI WA RASHID MATUMLA. Kila akiulizwa swali au akiongea kama simuelewí anaongea nini.
Jamaa naona ngumi zilimuathiri..
Hiki kitu hata mimi nilikinotice mkuu! Ile ongea yake nilihisi anatatizo au pengine nikahisi yupo maji/vyombo kama ni mtumiaji
 
Mwakinyo anapoteza hili pambano..

Anaruhusu Ngumi mno
Ngumi nyingi si tatizo, suala anapiga ngumi zenye point? Mpinzani wa Mwakinyo anapiga ngumi nyingi sana usipoweka gadi na kuwa mvumilivu wa gadi anakuondoa mapema sana. Ukipigana na mtu wa namna hiyo ni lazima umtafute na ndicho alichofanya Mwakinyo.

Ni kama Mayweather alivyopigana na Pac yao. Kwa sababu Pac yao ukimruhusu apige nawe upige anakuondoa. Kwa sababu anarusha ngumi nyingi sana. Kwa hiyo muhimu ni gadi yenye uvimilivu na unampiga sehemu muhimu.
 
Mwakinyo Will lose this fight aisee....mwakinyo anaruhsu sana kupigwa
Mwakinyo anachokifanya ile ndiye boxing sasa! Mwakinyo mrefu kidogo kwa yule Mfilipino na Mfilipino ameligundua hilo. Ukipigana na opponent ambaye naye ni bigger halafu ni taller than you ni rahisi kukupiga. Kwa sababu ya weight yake na mrefu zaidi yako kwa hiyo mikono yake ni mirefu kuliko yako. Mtu wa namna hiyo anao uwezo wa kupiga ngumi na ikaku' push. Hii kwa mwenye kimo kifupi ni disadvantage kwake.

Alichokifanya Mfilipino ni kutoruhusu Mwakinyo apige! Hakumpa nafasi hiyo! Kwa sababu Mwakinyo ni mrefu zaidi yake na ngumi zake nzito vilevile. Kwa hiyo akawa anapiga ngumi nyingi sana. Opponent anayerusha ngumi nyingi sana kwenye ring usipigane naye inside fighting.

Lazima atakazo rusha hata kama ukiweka guard kuna bomba lazima itakuumiza kwenye mikono. Itakufanya u' lose balance ya kwenye miguu na atakushambulia na atakuumiza.

Cha kufanya fanya kama Mwakinyo. Ziegemee kamba kwa sababu zinakupa support yaani unaziegemea huku ukiweka guard na haumruhusu akuchungulie sana. Unamkwepa kisha unamshitua na konde ya sehemu ya point.

Na huu upiganaji ndiyo anaopigana May weather. Mwakinyo yupo vizuri. Ila boxer mwengine ambaye ni hatari ni Mfaume. Mfaume ngumi yake ya kushoto ni nzito! Halafu haogopi anakufuata. Huyu jamaa ni hatari! Halafu anapiga kimahesabu.
 
Mlianza na samata mmemsema wee sa hivi zamu ya mwakinyo ameshakua hajui tena duu si wa Tz sijui tunakwama wapi aisee

Round 10 si mchezo kipindi nafundishwa boxing kwa ajili ya self defence nikjiona nshakua bondia nikapewa dogo mmoja hivi ni fight nae round 3 tu nikwambia mbona round ndogo fanya hata round 6 aligoma mpambano ulipoanza niliishia round ya 2 tena hata zile dakika 3 siku maliza nikasanda nilikula jab za kutosha nilipgwa moja ya tumbo nikakutanishwa na huki moja ya chini ya kidevu daah

msione mtu ana rukaruka ukazani kakosa pakupiga yaan ile we unaangalia upige wapi ushapigwa ngumi 2 za fasta

huo mpambano ni ngoma droo
 
Kuna vitu ulikua huangalii mkuu, nyingi ziliishia kwenye guard ya mwakinyo, hata alivyokua akikimbilia kwenye kamba ni mbinu mojawapo ya kumdanganya akishambulia kwa kasi anamlisha moja ya ukweli afu anajitoa ndio maana mfilipino alikua hajiamni anapomshambulia akiwa kwenye kamba.... Hii ni mbinu ya kiupigaji, km mwakinyo angekua anarudi nyuma kumuogopa basi pambano lingeisha mapema sana,
Matumla alionyesha hofu maana alijua anamuopa ndio maana alikua akirudi nyuma.. Kumbe zilikua mbinu
 
Unasema nini kuhusu kuanguka chini mwakinyo na mwamuzi akadao alisukumwa?
Alikua kwenye harakati za kukwepa ngumi ndio akaenda chini sio ngumi ilimpeleka chini hata ulaya tunaona sana hayo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…