Mwakinyo kuzichapa na Mzimbabwe Mei 28 mkanda wa WBC African Boxing Union (ABU)

Mwakinyo kuzichapa na Mzimbabwe Mei 28 mkanda wa WBC African Boxing Union (ABU)

Do santos

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
635
Reaction score
338
Bondia Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupigana na Bondia wa Zimbabwe Brendon Denes, kuwania Mkanda wa WBC Afican Boxing Union (ABU) uzito wa Super welterweight May 28 mwaka huu, katika ukumbi wa Next Door Alena.

Brendon Denes ana rekodi ya kupigana ngumi za Professional mapambano 8 kati ya hayo Matano ameshinda kwa KO na matatu kwa pointi.

Pia anashikilia Taji la WBF intercontinental uzito wa super lightweight aliloshinda 2019 nchini Namibia.

Ana umri wa miaka 26 na rekodi zake akiwa ngumi za Amateur amepigana mapambano 54, akishinda Mapambano 52, akipoteza mwaili tu.

Brendon Denes ambaye anafahamika kama 'Boika' ni msomi wa Shahada ya Politics Science and Public Administration katika chuo kikuu cha Zimbabwe.

Mwakinyo atapigwa au kapewa Bondia utelezi?
 
All the best

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom