post hii naileta hapa kwenye jukwaa la sheria nikiwa na matumaini kwa wanajamvi pamoja na mengine kunisaidia masuala ya kisheria imekaaje,.mimi ni mtumishi wa MAMLAKA YA RELI YA TANZANIA NA ZAMBIA TAZARA tangu mwaka huu wa 2013 uanze hatujawahi kupata mshahara,leo hii tunazungumzia ni mwisho wa mwezi wa tatu,.Waziri amekuwa anapita na ahadi za uongo kuhusu masuala mbali mbali ya shirika lkn tunaona kama kuna DUDU kali ndani ya IKULU linalo zuia utekelezaji wa mikakati kabambe ya utendaji,.juzi alipata taharifa za mabehewa kubeba mikaa na mbao suala ambalo alilipa uzito wa kisiasa kuliko pelekea kuja na waandishi wa habari usiku wa manane kuonyesha kuwa ni mtendaji lkn ni porojo tu,.suala la mishahara kwa wafanyakazi analipata kila kukicha tunaona analikwepa tu na ilidiriki mtu mmoja kumuambia siku alipokuja tazara akiongozana na waziri wa miundo mbinu wa zambia kuwa,.namnukuu,''mweshimiwa unatuambia treni hii ya jiji tusiisimashishe tuiache itembee lkn unajua kuwa wanayoiendesha hawana mishahara ya miezi mnne?,wewe sizani kama dereva wako akiwa amelewa unaweza kumruhusu akuendeshe sasa sisi tumelewa pombe mbaya sana,tumelewa njaa ya miezi minne na hapo unatusihi tuendeshe treni sasa huoni unahatarisha maisha ya watu hawa kwa kuendeshwa na watu wenye mawazo ya watoto wao kula nini,kutibiwaje,kusomaje,kulala nje ya majumba baada ya kufukuzwa kodi?''mwisho wa kunukuu,.waziri akaleta majibu ya siasa,.sasa ikaja wakakutana tena Lusaka zambia kwa suala la TAZARA ila WAZAMBIA wako COMMITED sana tatizo ni hapa kwetu,.najua kuna watu wa karibu wanapita humu nawaomba wamfikishie ujumbe huu maana njia zote tumetumia imeshindikana pia kwa kutumia TRAWU hasikii na wafanyakazi wenyewe nao wapi basi wanajukwaa wa karibu yake waongee nae,.na naomba usheuri wa nini kifantike ili kulinusuru shirika hili la TAZARA.:attention::attention: