Mwakyembe: Tunatunga Sheria ya kulinda hadhi za Watangazaji, kutakuwa na gharama za usajili kama kwenye mpira

Mwakyembe: Tunatunga Sheria ya kulinda hadhi za Watangazaji, kutakuwa na gharama za usajili kama kwenye mpira

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Waziri Mwakyembe jana akifanya mahojiano na TV ya mtandaoni kuhusu maoni yake kwa watangazaji kuhama vituo vyao vya kazi kila siku, Mwakyembe amesema Wizara inamalizia hatua za mwisho mwisho kuunda chombo kama TTF ya redio na TV itakayokuwa na jukumu la kulinda hadhi ya watangazaji.

Pamoja na mambo mengine chombo hiki kitakuwa na jukumu la kusimamia ada za uhamisho kwa watangazaji na maslahi mengine.

Mkuu toa maoni yako
 
nadhani ni wazo zuri kama litasimamiwa vizuri,asisahau na mishahara
 
....chombo kama kama TTF ya redio na TV itakayokuwa na jukumu la kulinda hadhi ya wachezaji, pamoja na mambo mengine chombo hiki kitakuwa na jukumu la kusimamia ada za uhamisho kwa watangazaji na maslahi mengine.
 
Hiyo ni media kubwa tu sioni kama itasimamia watangazaji wote nchini. Mtangazaji anatoka Kasibante Fm anaenda Kifimbo Fm na njaa hii mtaanza kufuatilia kama kweli kapewa ada yake?

Hii tasnia ina njaa kali sana ni kama mpira wa miguu ulivyo hapa nchini. Mtangazaji atafanya makubaliano na kule anapoenda iwe kwa kupewa ada au mshahara mzuri ataondoka kisa NJAA.

Umeitwa media B uje wakulipe mshahara wa 1m wakati media A ulikuwa unalipwa 500k unaachaje kuondoka bila ada. Sioni mafanikio yoyote kwenye hili. Media nyingi hapa nchini zinatembelea magoti.
 
Kama naona vile kifuatacho ITV katika breaking news ambayo mtangazaji atashangaa kwanini mdomo unatetemeka kutangaza.
 
....chombo kama kama TTF ya redio na TV itakayokuwa na jukumu la kulinda hadhi ya wachezaji, pamoja na mambo mengine chombo hiki kitakuwa na jukumu la kusimamia ada za uhamisho kwa watangazaji na maslahi mengine.


Kwa mtazamo huo basi hata madereva wa malori waundiwe TFF yao.
 
1. Media iwe limited kusajili idadi ya watangazaji kutoka chombo kimoja kwa msimu mmoja.
2. Ada ya uhamisho iwe kubwa na serikali ipate kodi.
3. Kuwe na adhabu ya kufungiwa kusajili pale media inapotumia pesa nyingi kusajili. Adhabu iwe kutokuruka hewani kwa mtangazaji husika.
MAONI YA MLEVI MMOJA KUTOKA MWANANYAMALA KWA KIDILE
 
Nafikiri hii ni sahihi sana. Kuwe na utulivu.
 
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameshindwa kura za maoni Jimbo la Kyela Mkoa wa Mbeya na kuwa watatu kwa kupata kura 252 dhidi ya Mshindi Ally Mlagila Kinanasi aliyepata kura 502 na Mshindi wa Pili ni Hanta Mwakifuna amepata kura 288.
 
Back
Top Bottom