Mwakyembe: Utake usitake, Diamond ni balozi wa Tanzania kwa kila kitu

Mwakyembe: Utake usitake, Diamond ni balozi wa Tanzania kwa kila kitu

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
DZWaFs_W0AAGJmC.jpg

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema msanii Diamond anafaa kuwa balozi wa maadili kutokana na ushawishi alionao kwa sasa.

Waziri Mwakyembe amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha watu wa Wizara hiyo, kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na menejiment ya msanii huyo ambapo walijadili mvutano uliojitokeza mara baada ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa.

“Ndio balozi wetu, balozi wa maadili pia, kwa sababu Diamond utake usitake yeye ni balozi wa Tanzania kwa kila kitu na safari hii tumemuomba hata maadili awe balozi wetu, kwa sababu watu wengi wanamfuta Diamond, yeye ni Super Star na tunajivunia Watanzania,” amesema.

Pia Waziri Dkt. Mwakyembe amesema maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara, hivyo ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa na Naibu Waziri Shonza hivi karibuni zilikuwa za Wizara kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Nawaagiza watendaji wa Wizara na Taasisi zake ikiwemo BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA, kuweka madaraja ya kazi zetu za sanaa, kuna kazi za sanaa ambazo kuonekana ni kuanzia saa sita hadi saa 12 asubuhi na hii inafanyika nchi nyingi ndio maana nimesema wakae na wenzetu,” ameongeza.

Source: Bongo 5
 
Si nimesikia wameagiza nymbo zake zilizofungiwa zifunguliwe mara 1??
 
Wasomi wa Tz bana... Huyu yupo kwenye level ya PhD...ukiwakuta humu wakijisifia mara udsm mara SUA mara Mzumbe... Nk.. Lakini angalia product zao sasa.... Heheheheee
 
Diamond yuko juu....juu....juu zaidi!
 
Wasomi wa Tz bana... Huyu yupo kwenye level ya PhD...ukiwakuta humu wakijisifia mara udsm mara SUA mara Mzumbe... Nk.. Lakini angalia product zao sasa.... Heheheheee
Elimu ya Tanzania ni kukariri yale tuliyoletewa na wazungu, ndio maana katika hili sakata mwanafilosofia wa ukweli ni Diamond umeona alivyowapeleka!
 
Elimu ya Tanzania ni kukariri yale tuliyoletewa na wazungu, ndio maana katika hili sakata mwanafilosofia wa ukweli ni Diamond umeona alivyowapeleka!
He he he he
Mkuu leo utanyimwa posh aiseee.

Unkwenda against na wakubwa publicly??
 
Hapa wamedhihirisha double standard ya kiwango cha juu kabisa.
Kuna watu wamefungiwa kufanya mziki pasipo hata kusikilizwa na hata baada ya kuomba msamaha bado hawajasamehewa.
Kweli hakuna usawa wala ubinadamu wote ni sawa.
Sema diamond kawakomesha
 
Naona aliopiga nao picha wanaonekana wako well fed,
sijui ndo kitimoto au kitu gani..
Hali pozi sasa..
Huyu kijana sijui huwa anakula mboga mboga tu,yaani mwili wake haubadiliki
 
kwa hiyo diamond anatuwakilisha watanzania na visarawili vyake anavyovaa..??huyu waziri boya nini??
angesema anawawakilisha wavulana wa dar akina bashite n.k hapo kidogo angeeleweka..
 
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema nyimbo mbili za Diamond, hazijafunguliwa kama inavyodhaniwa.

Akizungumza na MCL Digital, leo Machi 28, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema nyimbo za Wakawaka na Hallelujah hazijafunguliwa na jambo hilo halina ukweli wowote na kuwataka wananchi kulipuuza.

Kadhalika, Mngereza ametoa ufafanuzi kwa nini msanii Diamond amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza na sio wasanii wengine.

Mngereza ametoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa taarifa iliyoeleza msanii huyo kakutana na mawaziri hao.

Baada ya taarifa hizo, kulizuka gumzo mitandaoni ambapo watu walihoji kwa nini wakutane na msanii huyo wakati kuna waliofungiwa nyimbo zao kama yeye na wengine kufungiwa kufanya muziki kwa miezi sita.

Mngereza amesema hatua hiyo imetokana na majibizano yaliyokuwa yanaendelea kati ya Diamond na naibu waziri Shonza na ndio sababu iliyowafanya wawili hao wakutanishwe meza moja ili kuyamaliza.

Akihojiwa katika kituo cha Redio Times FM, Diamond alisikika akimrushia maneno moja kwa moja Shonza kuwa amekuwa akiwafungia wasanii nyimbo zao na kuwafungia wasifanye kazi kwa lengo la kutafuta umaarufu na kuogopa kutumbuliwa.

Hata hivyo, kwa upande wake Shonza alisema hayupo tayari kujibizana na msanii huyo mitandaoni kwa kuwa aliyemfungia si yeye, bali ni serikali na kumtaka kufuata taratibu kama anaona ameonewa ikiwemo kufika Basata, Wizarani au kuandika barua, jambo ambalo Diamond alilitekeleza siku ya Ijumaa.

Akizungumzia hilo, Mngereza alitaka wananchi waelewe kwamba malumbano hayo ndicho chanzo cha Diamond kukutana na mawaziri hao na kuwataka kuondoa dhana kama mtu aliyepewa upendeleo katika sakata la kufungia nyimbo.

Alipoulizwa kuhusu kukutana na wasanii wengine wenye malalamiko amesema mpaka sasa hajapata barua yoyote ya wasanii hao kutaka kuonana nao.
 
Diamond ndio Sanaa Utamaduni na Michezo ile ni wizara tu,ila Bongo Bahati Mbaya samahani Jk najua tulikukosea pale si patamu tena
 
Back
Top Bottom