Mwakyembe: Wanachama wa vilabu vya michezo kumiliki 51% ya hisa na wawekezaji 49%!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hiyo ni kwa mujibu wa sera mpya ya michezo ambapo kanuni zake zinaandaliwa na mamlaka husika.

Chanzo: TV 1 habari!

My take Mo wa Simba SC atapona kweli?!!
 
Basi sina haja ya kumlaumu Kinje kumbe matatizo yanaanzia huku
 
Sijui serikal ina hofu gan ktk hivi vilabu..mbona yenyewe inauza mashirika yake kwa asilimia zaid ya 50. Kuna wakat naamin serikal ndo inadumaza michezo kwa sera za kizamani kama hizo.
wanahofia ya tp mazembe na moise katumbi au manji kwa yanga kabla hawaja mblock,mtu anakuwa powerful hadi kuabudiwa na mashabiki zaidi ya serikali
 
Basi sina haja ya kumlaumu Kinje kumbe matatizo yanaanzia huku

Hawa hawana ajenda, wamebaki kurukia tu issues. Watafakari kuboronga kwa timu ya taifa na kili stars mambo ya business developments za vilabu siyo priority issue kwa sasa.
 
wanahofia ya tp mazembe na moise katumbi au manji kwa yanga kabla hawaja mblock,mtu anakuwa powerful hadi kuabudiwa na mashabiki zaidi ya serikali

Mwaka 1975 wakati Yanga imetolewa na Enugu Rangers na kutuhumu wachezaji wakongwe kutumiwa kuhujumu ili coach mkongo marehemu Tambwe Leya afukuzwe, mgogoro mkubwa ulizuka na habari za ki intelijensia zikaonyesha kuwa kulikuwa na mkono wa kisiasa hivyo Tambwe Leya alipewa muda kuondoka nchini.

Sasa Simba kulikuwa na Coach wa maana kutoka Guinea Conackry, marehemu Naby Kamara, ikaamuriwa naye aondoke nchini eti makocha wa kigeni wanasababisha migogoro na hata kujiingiza kwenye siasa et.c.

Simba ilipata hasara katika benchi la ufundi kwa sababu ambazo kwa jicho langu enzi zile zilikuwa za kuikomoa au ku-balance kati ya hawa watani/mahasimu! kama kuna mtu ana version nyingine ya tukio hili anisaidie.

Nina mashaka kuwa hii tabia haijaisha. Mdogo wako, pacha wako au kaka yako hana nguo za krismasi au Idi, ngoja kwanza mpaka naye awenazo ndiyo mzivae.

NAHISI NDIYO KINACHOENDELEA.
 
Sheria /kanuni mpya haiathiri mikataba ya nyuma yaani ile iliyofanyika kabla sheria hiyo haijatungwa.

Amini nakwambia hii sheria ikiwa active, vilabu vyote vya wanachama vyenye umiliki wa wanachana usiozidi 51% vitashurutishwa kufanya marejeo ya mikataba na wanahisa wake....

sheria haibagui mkuu.

Kwa hivyo hili jambo likiwa tayari kutekelezwa na vilabu, MO inabidi awe mnyonge tu na akubali kumiliki 49%.
 
Nasubiri kwa hamu hao wanachama wataojitokeza kununua izo hisa asilimia 51zenye thamani zaidi ya billion 20 alizotoa mo !
 
Nasubiri kwa hamu hao wanachama wataojitokeza kununua izo hisa asilimia 51zenye thamani zaidi ya billion 20 alizotoa mo !

bilioni 20 ni sawa na shilingi 40,000 kwa watu laki tano ( 500,000), au kwa shilingi 20,000 kwa watu milioni moja. Nilifikiri thamani yote ya klabu ilivyothaminiwa pamoja na pesa ya MO italetea thamani ambayo portion yake ndiyo asilimia hizo 51%/50%/49%, ambapo kuna kundi (Kilomoni or else)lililopewa asilimia kadhaa may be bure: limetengewa, alafu asilimia zinazobaki ndiyo kwa ajili ya kununuliwa na wanachama.

Ni muhimu kuona document kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…