Mwaliko wa wadau kutoa maoni mbele ya kamati ya bunge ya katiba sheria

Mwaliko wa wadau kutoa maoni mbele ya kamati ya bunge ya katiba sheria

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801


MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA BORA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI
(THE CONSTITUTIONAL REVIEW BILL, 2011)

Kwa mujibu wa Kanuni ya 114(9) ya kanuni za kudumu za Bunge, kamati ya Bunge ya Katiba, sheria na Utawala Bora inawaalika wananchi na wadau wote kushiriki katika mkutano wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya katiba ili kupata maoni na ushauri wao kwa ajili ya kuboresha Muswada huo.
Mikutano ya kupokea maoni hayo itafanyika tarehe 7, 8 na ikibidi tarehe 9 April, 2011 Mjini Dar es salaam na Dodoma kama jedwali hapa chini linavyoonyesha:

S/NSIKU MKOA UKUMBI
MUDA
7 – 8/April/2011Dar es salaamKarimjeeSaa 3 Asubuhi7 – 8/April/2011DodomaMsekwa








Kwa taarifa hii, wananchi wote kwa ujumla wanaalikwa kushiriki kwenye mikutano hii kwa ajili ya kutoa maoni yao kama inavyoonekana katika jedwali hapo juu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Dar es Salaam
5 Aprili 2011
 
Back
Top Bottom