MWALIMU AAMUA KUFUNGUKA UKWELI WA MAISHA YAKE....Je kwa hali hii watoto wanafundishwa kweli?

MWALIMU AAMUA KUFUNGUKA UKWELI WA MAISHA YAKE....Je kwa hali hii watoto wanafundishwa kweli?

Kimetah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
1,049
Reaction score
189
BARUA YANGU KWA RAIS.(Serious).Habari yako mheshimiwa Rais?Kwanza kabisa heshima yako,shikamoo na Pole sana na kazi zakulitumikia Taifa letu. Mimi ni mwalimu wa shule ya msingiMatakapola, iliopo Ilala hapa Dar.Haina aja ya utambulisho sana,naomba niende kwenye dhumuni la hiibarua.(Ila ombi, naomba hii baruausome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishiehapa. Aiweke store siku ukiwa namuda wa ziada wewe ndio isometaratibu. Tafadhali sana).Ijumaa iliopita mshahara wanguuliingia kwenye account yangu. Asante sanaingawa ni jasho langu.Basi yafuatayo ni matumizi yanguyangu tokea Ijumaa hadi leo:1. Kodi ya chumba (miezi 3)-Tsh60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh.5,0002. Chakula cha akiba kwa huu mwezi(Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage5kg, Mafuta 2lts)-Tsh 42,000.3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vituvidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi,mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,0004. Mwalimu usafi, imebidi nipitiemitumbani (huku ni sehemuunakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa beinafuu) nipate nguo za kubadilisha,maana hizi wanafunzi wamenizoeanazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000na nkazipeleka kwa fundikuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani nikawaida kua oversize, ombea isiweundersize, na ukishanunua hakunaguarantee wala kurudisha) hapankatumia tena Tsh 5,000.Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5000), Mafuta yaBabyCare (Tsh.1000).5. Wazazi wangu wameteseka sanakunisomesha, hivyo fadhila muhimukuwarudishia kwa hiki hiki kidogonipatacho. Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumiekubadilisha mboga juma pili na nusuiwasaidie kumalizia ada ya mdogowangu Riziki, yupo ile shule uliokujaizindua mwaka 2011/May/13 kijijinikwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka,maanaulituhaidi visima, barabara, madawatishuleni na kujenga bweni lawasichana, ila hadi leo umetuachiamanyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati ladrafti drafti jeupe. Na ulikuja namama, yeye alivaa full vitenge vyachama! Kumbuka?)6. Kuna hela ya nauli kwenda nakurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku(Tsh.200 per day), na vitu visivyonunulika kwa wingi, maanavitaharibikakama vitunguu, sabuni, nyanya,nazi,karoti, etc nakadilia Tsh.10,000 kwa mwezi.7. Mheshimiwa kuna vitu havizuilikikama vocha, nyama wakija wageni,kwenda hospitali, bado kutoka outmara moja moja (Yaani kama weweunavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaendaga kwa mama Lucysinza, kula vifaranga).8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela yaemergence kama michago ya mtaani,sadaka, misiba, kiatu/nguo kwafundi...etc Mheshimiwa kama ulisoma vizurihesabu kama mimi, roughly hapo nijumla kama Tsh.210,000 nikiongeza napesa ya hitaji no.7&8 jumla kamaTsh.250,000.Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakua mamahapo nyumbani ameshawahi kuamwalimu naomba nikusumbue, ebumuulize walimu grade A, tunaoanzakazi tunalipwaje?Kumbuka hapa bado niko peke yangu (Single Boy), sina ata mpenzi. Hivi nnandoto za kuoa kweli ukitizama ikokipato? Nikiwa na mtoto je? Akianzakusoma je?Nawaza sijui nikakope NMB au FiNCAau VICOBA sijui Bay Port au SACCoS?Yaani sijielewi. Sikushawishiuniongeze mshahara, ninachoomba tu,fananisha kazi yangu na hiyowanayofanya wabunge "wako"niliowachagua, au ata kazi unayofanya wewe.Ndio.Wewe Mheshimiwa.Kuna watu wananishauri nianzishetuition, lakini mimi ni mzalendo wa pilibaada ya Nyerere, itakuaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this isnot fair (Sijui kama umeshawahi wazaili Mh.)Wengine wamesema nianzishebiashara. Sijui hata pa kupata mtaji,pili sio vizuri maana ntaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi yakuelimisha ili Taifa, narudia tena mmMzalendo.Hawa waliosema niache kaziwapotezee (achana nao).Ok Mh, naomba nisiongee sana maana unakazi, safari na mambo mengi sana.Nisikuchoshe.Natumaini ombi langu (Kamaumesahaula kuweka hapo matumizi yako yamshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi.Wako katika kujenga, kuelimisha nakuandaa Taifa lijalo

 
Ilishakuja humu mwaka juzi na tuka comment sana..
 
Back
Top Bottom