BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma mkoani Mara, imemuhukumu kwenda jela miaka 30 mwalimu Idrisa Athumani (29) wa shule ya Msingi Kyawazaru iliyopo wilayani Butiama baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake
Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 16,2022 ikiwa ni siku mbili tu tangu mwalimu huyo kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Musoma baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti mwanafunzi mwingine.
Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley amesema kuwa mahakama hiyo imejiridhisha pasi na shaka kuwa mwalimu huyo aliyeajiriwa Desemba mwaka 2020 na kuanza kazi shuleni hapo Januari, 2021 alitenda kosa hilo kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.
"Mahakama hii inakutia hatiani kutokana na kosa uliloshtakiwa nalo na ili iwe mfano kwako wewe na wengine wenye tabia kama yako ukizingatia kuwa umekabidhiwa watoto ili kuwatunza na hili suala ni kinyume na tamaduni zetu, halitakiwi wala kuruhusiwa nakuhukumu kwenda jela miaka 30" amesema
PICHA: Mwalimu Idrisa Athumani Najela