Mwalimu akizushiwa uongo afanyeje?

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
895
Reaction score
571
Ndugu wana JF. Kwanza pokeeni salamu zangu. Napenda kuwauliza endapo mwalimu wa shule ya sekondari amezushiwa uongo na mkuu wa shule kwamba anawakusanya wanafunzi na kuwachochea ili wafanye fujo shuleni huku afisa mtendaji wa kata akisema kwamba mwalimu huyo aliwaingilia polisi kutekeleza majukumu yao ya kuwaadhibu wanafunzi waliokamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Habari hizo hazina ukweli wowote maana polisi walikanusha kuwepo kwa taarifa hiyo na shuleni, pia wanafunzi na walimu shuleni walishangazwa na taarifa hizo. Je, mwalimu huyo anatakiwa kuchukua hatua zipi dhidi ya watu hao wawili waliomzushia uongo na kumchafulia jina lake? Nawaachia wanajukwaa mselebuke kwenye sakata hili.
 


Wapigwe tu, mi nasema wapigeni tu sasa tumechoka.
 
Hiyo shule ni ya private or government??ukinijibu hili nakupa njia?
 
Hiyo shule ni ya private or government??ukinijibu hili nakupa njia?



huyo bwana hana lolote,, kwanini yeye tu?? kwani ndiye mwalimu pekee hapo shuleni? isitoshe atakua anajipendekeza kwa wanafunzi. aache hyo tabia ya kua karibu na wanafunzi, pumbafuuuu
 
kusanya vielelezo kuntu, halafu uvitumie kama ushahidi mahakamani. namaanisha kuwa, ufungue kesi ya madai ya fidia ya kuchafuliwa jina/sifa.
 
huyo bwana hana lolote,, kwanini yeye tu?? kwani ndiye mwalimu pekee hapo shuleni? isitoshe atakua anajipendekeza kwa wanafunzi. aache hyo tabia ya kua karibu na wanafunzi, pumbafuuuu

Habari zilitotolewa ni za kuzushiwa uongo. Hakuna ukweli kuhusu taarifa zilizotolewa na mkuu wa shule pamoja na afisa mtendaji wa kata ndio maana mwl huyo anatafuta msaada wa hatua za kuwachukulia hao watu waliomchafulia jina lake. Hapa nchini tunaishi kwa kuzingatia taratibu za nchi. Kumzushia mtu uongo ni kosa la kisheria. Nashukuru kwa maoni yako mazuri pamoja na lugha safi uliyotumia. Mungu akubariki uendelee kuwa hivyo hivyo kama jinsi ulivyo na fikra zako njema zidumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…