vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
[h=2][/h]
Ndugu wana JF. Kwanza pokeeni salamu zangu. Napenda kuwauliza endapo mwalimu wa shule ya sekondari amezushiwa uongo na mkuu wa shule kwamba anawakusanya wanafunzi na kuwachochea ili wafanye fujo shuleni huku afisa mtendaji wa kata akisema kwamba mwalimu huyo aliwaingilia polisi kutekeleza majukumu yao ya kuwaadhibu wanafunzi waliokamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Habari hizo hazina ukweli wowote maana polisi walikanusha kuwepo kwa taarifa hiyo na shuleni, pia wanafunzi na walimu shuleni walishangazwa na taarifa hizo. Je, mwalimu huyo anatakiwa kuchukua hatua zipi dhidi ya watu hao wawili waliomzushia uongo na kumchafulia jina lake? Nawaachia wanajukwaa mselebuke kwenye sakata hili.