Mwalimu auawa kikatili tena Dodoma wadau, hii inaogopesha

Mwalimu auawa kikatili tena Dodoma wadau, hii inaogopesha

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Screenshot_20220206-035053_Drive.jpg

Mwenye ripoti kamili ndugu zangu.
Tuna shida. Tunahitaji uponyaji.

Hii inaogopesha.
 
Mamlaka zitenge siku ya kutoa taarifa za vifo ili kupunguzia watu msongo wa mawazo.

Taarifa za vifo zinarindima kila kukicha na kuwathiri watu kisaikolojia.

NB: Kuna watu walidhani mikoa fulani ndiyo huu watu. La hasha, makabila yote kuna mauaji. Usihukumu ukaja kuhukumiwa.
 
Tumefikajefikaje kwenye hali hii!??
 
Tumefikajefikaje kwenye hali hii!??
Matumizi ya sheria bila busara. Kuna wataalamu wa sayansi ya jamii wamepuuzwa. Jamii inahitaji social healing.

Kukamata na kusweka rumande siyo suluhu ya kudumu na pengine, inachangia hali kuwa mbaya zaidi.
 
Kweli kabisa
 
Tumefikajefikaje kwenye hali hii!??
Unajua hujui ni msemo wa wanajamii kwa kweli ni bora kukutana na simba ambaye uwezekano wake mkubwa ni kukujeruhi ama kukuua kabisa lakini sio hawa binadamu kwani mchana ni watu lakini usiku ni watu walio ndani ya ngozi ya chui.
 
Matumizi ya sheria bila busara. Kuna wataalamu wa sayansi ya jamii wamepuuzwa. Jamii inahitaji social healing.

Kukamata na kusweka rumande siyo suluhu ya kudumu na pengine, inachangia hali kuwa mbaya zaidi.
So watanzania wako frustrated...wako na deep hate....full of rage..disapointment and revenge,, jumlisha na umasikini wa kupwaa.
 
Masuluhisho mengine yanashangaza, unang'oaje mti wa mzabibu utoao punje za dhahabu na kupanda maharagwe ili uchume majani yake kwa ajili ya kupata mboga za majani.
====
Kama taifa, haraka sana tutatue tatizo hili bila mihemuko. Nyeupe iwe nyeupe na nyeusi iwe nyeusi.
 
Watanzania wengi ni wagonjwa wa akili .
 
So watanzania wako frustrated...wako na deep hate....full of rage..disapointment and revenge,, jumlisha na umasikini wa kupwaa.
Humanity ubinadamu hamna.

Hili limekuwa hivi kwa sababu wengi tumeelemea spiritual beings haswa ushirikina. Cha kushangaza, baadhi ya makanisa wamekuwa kama wapiga ramli chonganishi.

Binadamu katika jamii ana nguzo nne: imani, akili, hisia na physical being. Hizi hufanya kazi kama miguu ya stuli ambapo kimoja kikizidi mtu (stuli) lazima awe na kasoro tu.

Utaona sasa jamii yetu imeegemea sana kwenye imani aidha ushirikini na au dini za kisasa.

Hii inachagizwa na hisia. Wengi wetu tunaishi kwa kutegemea hisia badala ya uhalisia. Mfano, mtu akifa, halafu nyumba ikajengwa; utasikia tuhuma (hisia) kwamba fulani kamuua yule (imani) ili apate mali. Hapo utaona kilichobaki ni akili (nguzo ya tatu) kuamua na hatimaye nguzo ya nne (physical being) inasubiriwa kuamua na hapo ndipo mauaji yanatokea.
 
Back
Top Bottom