joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ila wakenya wamezidisha ukatili sana, ukifuatilia mauaji yanayofanyika Kenya, huwezi amini kama wakenya wamefikia unyama kwa kiasi hiki, karibu kila siku watu wanauana kwa sababu za kijinga sana. Kwa ufupi wakenya inaonekana wana "frustration" nyingi sana za kimaisha, kama walivyo " Black Americans" huko USA.jambo hili limenitia hasira sana.. mama ya mtu anauawa na watu kinyama hivyo kwa sababu zisizo na msingi wowote
Kwanini hutumii busara katika kujenga hoja?. Tunaposema Marekani ni tajiri, haina maana kwamba hakuna masikini, tunaposema Africa ni masikini haina maana kwamba hakuna matajiri, tofauti ni wingi wa watu matajiri ukilinganisha na watu masikini.Tusiisemee Kenya kwa mauaji ya hovyo ikiwa hapa kwetu watu wanachinjwa hadi familia nzima,wamama wanaua waume zao kikatili,nyumba zinachomwa moto zikiwa na watu ndani,watoto wadogo wanauliwa kinyama na watu wanatupwa kwny viroba bila idadi kamili.
Sent using Jamii Forums mobile app