Mwalimu awa fundi viatu! Duh!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,986
Reaction score
5,058
Kwenye taarifa ya star tv wamemuonesha mwalimu mmoja wa shule ya msingi ambaye anafanya kazi hiyo baada ya masaa ya kazi. Nimesahau jina na halmashauri yake. Imeniumiza sana kwa kweli, tena anasema kabisa maisha yamemuwea magumu. Poleni shemeji zangu! Nchi yenye kila utajiri wa kuwalipa mishahara hata wasiofanya kazi lakini wanapewa madaraka majangili wa siku zote.
 
Si ndio ujasiriamali huo jaman au?
 
Si ndio ujasiriamali huo jaman au?

ninachosikitika ni kitendo cha kazi yake kuwa ngumu lakini mapato yamemuwea adimu kiasi cha kuingia kwenye kazi ambayo hata kijana smart asiye na kazi huwa tunaidharau. Ndo maana hata mwalimu akifungua mashamba huwa inakuwa tofauti na mkulima wa kawaida. Mf huwa wanaajiri vibarua wa kutosha, njia bora za upandaji na mavuno huwa bora kuliko wale wengine. Sasa ndugu yangu duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…