Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
salaam wana.jf
kuna mtu wangu wa karibu kaletewa cheti cha ualimu ila kimeandikwa daraja A. je,hilo daraja ndio linafaa kufundishia au nini?
__anaweza kuajiriwa ualimu?
na je waalimu wanaajiriwa na nani?
Mtu wako wa karibu ndiyo nini? Sema kama ni demu wako. Haya, Mwalimu daraja "A" ni yule aliyemaliza kidato cha 4 na kusoma Astashahada ya Ualimu (Certificate in Teaching) Kwa mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo (Education and Training Policy) ya mwaka 1995, mwalimu wa daraja "A" anaruhusiwa kufundisha katika shule za msingi tu.
Anaweza kuajiriwa na serikali au wenye shule binafsi kama sio kilaza.
Walimu wana waajiri wengi, Serikali ya Tanzania (kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mamlaka za Serikali za Mitaa,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nk), mashirika ya dini, watu binafsi nk
kwa hiyo wakuu
ni taratibu gani za kufuata ili kupata ajira?