Mwalimu gani mkali ushawahi kukutana nae katika maisha yako ya shule...!!!??

1988 to 1991, form 1B, form 2 to form4 group 4 electrical.... Halafu kula na kocha, ticha wa bweni la chabu huyo, halafu kulikuwa na Lihuruku a.k.a Mbungi, si mchezo

Duuh mkuu shikamoo hata sijazaliwa bado yaan una malza 4 me nna mwaka 1
 
Mwalimu njowoka! Kiboko

Dah umenikumbusha huyu mwl alinitandika bakora sana mwanzo wa tuishen mpaka namaliza. siunajua njowoka alikua hatak uchafue daftari,hakuna kukata ukikosea,hakuna kuchana karatasi, na daftari likiisha unaliunganisha na lingine hata daftar 6 tena yamejaladiwa, na hakuna kukosa swali wala kuacha swali likikushinda na madaftari yanatakiwa mapema sana yakusanywe kabla somo halijaanza.

Lenyewe linakaa nje kwenye dawati linasahihisha na moustach wake mzito, pembeni ana kopo moja usawa wa kufika magotini lililojaa maji yaliyotapakaa pilipili na rundo la fimbo.

Ogopa hapo kila mtu darasani yupo kimya anajisomea mana kuongea kutasababisha kutembea kwa bakora baada ya kupata majina kutoka kwa wanahabari wake monitor na monitress lasivyo nao wasipotaja hayo majina kiama cha bakora kitawatembelea.wakati huo linapitia daftari moja baada ya lingine,( kila
Siku unapewa maswali kama50 hivi ukafanye nyumbani) na likishamaliza kupitia linakuita ukachukue daftari.
sasa omba usiwe umekosa swal kwani kila kosa moja unapata bakora moja umechafua au umekata lakini umepata swali bado utakula bakora moja kwa kila uchafu wako, sijui hujajaladia ni bakora tu,karatasi imechanika au umechana baada ya kuona umekosa mtatambuana pale.
Hiyo ndio ilikuwa tuishen zinazojenga nidhamu,umakini kwenye kufanya mambo yako na kutafakari kabla hujatenda, kwani tulikua makini sana kuhakikisha hatukosei wala kuchafua daftari Kwa kukata au kufuta, kwani matendo yote hayo yana adhabu na kutufanya na sisi tujitahid kwenda na standard za mwl wetu kwani ndiye anayetuelekeza namna ya kuwa bora.
na vilevile alinijengea mazoea ya kuweka kumbukumbu zangu za masomo. Nilipoanzia mpaka nilipoelekea( development process yangu).
Alikua mwl mzuri sana kwani wengi waliosoma kwake walikua wanafaulu mitihani ya darasa la 7
RIP MWALIMU NJOWOKA
 
Mkuu, ongezea na Olu wa kiingereza fomu one, kulikuwa Mchili bana akianza next next next mtakoma na hesabu zake.... Kitomali duh.

Ila mwalimu poa alikuwa Kinyakanyaka, akianza kukuchara fimbo, ukitoka nduki yameisha...

Enzi zetu palikua na imani mbaya sana kwamba kila anapokua zamu Olu lazima tukiolisilokua la kawaida litokee.
Miaka uliyopita hapo imenifurahisha mkuu. Sie wajuzi juzi tu.

Nilikua group 4 Electronics, uzuri wa group 4, unaweza kuwa wa kwanza leo na mtihani ujao haupo hata kwenye 10 bora!
 

alikuwa anakuwahisha ukafanye adhabu
 

unaonekana ni rahisi kuhongwa misosi...
kayaman
 
uliposema samora, umenikumbusha lizaboni, kakululu bar, foloma... Maana wakati tunasoma hata dalili za samora hazikuwepo... Lile eneo kulikuwa kuna kitu tunakiita ''' luhanu'' kikwetu


mkuu Ngalikihinja,sasa sisi tulikuwa tunacheza mpira pale kanisani(kigangoni) jirani na mzee ngalikihinja au baba mponjoli,kulikuwa na mbwa anaitwa bobi alikuwa mkali balaa mpira ukisogea kwake anauchukua anampelekea mzee.

Unamkumbuka mpomoli,mzee nkoma,mzee zenda(apunene)

vipi mitaa ya kwa sudi,kwa mzee japhari na msufini?
Nimekumbuka mbali pia ulipotaja LUHANU ukicheza nao vibaya lazima ukukate.
 
Last edited by a moderator:
nimemsahau jina, alinichapa bakora za mgongoni almost kila kipindi maadam mmoja alikuwa mwalimu wa hesabu darasa la tano (mwenge p/s mwnz). nilikuwa nashindwa maswali ya kuzidisha namba nyingi. Hadi leo kwa sababu yake sijawahi kufeli tena hesabu au somo lolote lenye hesabu popote pale tenaa.

ukali wake ulinisaidia
 

Na ID yangu naitumia kwa sababu ya Mzee Ngalikihinja, maana alikuwaga ananilazimisha sana kucheza Mganda pale pale Kigangoni... Na alikuwa ana mtoto sister Fanikio, akina Mponjoli, Deo...... Unamkumbuka mzee Sisiru..?? Mzee Japhari (RIP) namjuwa sana, ana mtoto anaitwa Kadoda, Mauwa (RIP). Unamkumbuka mzee Henjewele..?? Unamkumbuka mzee Magogogo..?? Unamkumbuka kadakuwima..??? Apunene bar naikumbuka sana.. ilikuwa mbele ya kwa akina Dagi, mama yao alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Huduma.... Unamkumbuka supershort..??? Unamkumbuka Mzee Masiwawa (Baba Tina)..??? Unamkumbuka Mzee Kolobiniani..?? Unamkumbuka Mzee Kawango..?? Unamkumbuka Mzee Kahanju..?? Unamfahamu Kafolo... we acha tu bana... YAANI KULIKUWA KATEKISTA MAARUFU wa shule ya Kiburang'oma, Misufini Majengo na Majimaji, TADEI KAYOMBO (RIP)
Unamkumbuka mama ANDUNJI....???
Sasa Sudi (au Mbambamba, alikuwa anashinda sana kimaduka na mtoto wa kahanju na wote walikuwa pale kwenye kona kuelekea sokoni) na kwa sasa amemuowa KACHIKI mtoto wa mzee Hamadi.

Unamkumbuka mzee Nyirenda (Dokta Nyirenda)..??


Kulikuwa na MBWA anaitwa SHIDA....ulishawahi kumsikia..??? Ngoja niishie kwanza hapo... UNIKOMBWISI KUTALI SANA..

 
Jaman tcha we2 albart ivumwe high school yan had sura yke ilkuwa km mzee kwajl ya kupga.
 
Mwalimu Saidi-ni mwanamke,huyu mama alikuwa maarufu kwa shule za msingi wilayani kinondoni,mi nilizijua mbakora zake shule ya msingi mwananyamala

Mwalimu Mbogoro,hapo hapo shule ya msingi mwananyamala b,mbakora zake akikuchapa j3 zinauma hadi ijumaa!
 
 
1976 - 1982 - Mwalimu Janeth (Kashasha Primary Skuli)...! "Swali | Kazi | Jibu ... Kaazi Kwenu"
 
Msasa akiwa Mazengo Tech sec sch na baadae akahamishiwa Nsumba noma huyo.

KAISHOZI wa Dodoma Sec yeye akikuta mwanafunzi wa shule yoyote anafanya ujinga mtaani ni stick tu alikuwa anatembea nazo kwenye Defender yake nyeupe.
 

nilikuwa ifunda 93-97, form three group 3 tulikuwa tunajiita free free boys kama sijasahau drs letu lilikuwa na msichana mmoja tu. nilikuwa mtaalamu wa kushinda lyande, msitu wa tembo na kukumbilia darini mwl anapokuja bwenini,balozi wa c6 mirambo.
nilikuwa naenda drsn kufanya mitihani tu, siku moja Olu akanikuta drsn akaniuliza kama nasoma drs hilo nikasema ndio akaniambia niende ofcn kwake akanihoji kwa kirefu mwisho akagundua sijawah kuingia kipindi chake, alinichapa fimbo sita yn ananichapa moja anasema kaa ipoe, ikipoa anachapa nyingine hd zilipofika sita, sitasahau siku hiyo maana nilishakwepa mengi lkn Olu alinidaka na kunisulubu vzr.
sasa Olu ni jrn yangu na ninamuheshimu sn ingawa sijawah kumwambia mbio zng zote ifunda yy ndo alikuwa ukingo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…