Dah umenikumbusha huyu mwl alinitandika bakora sana mwanzo wa tuishen mpaka namaliza. siunajua njowoka alikua hatak uchafue daftari,hakuna kukata ukikosea,hakuna kuchana karatasi, na daftari likiisha unaliunganisha na lingine hata daftar 6 tena yamejaladiwa, na hakuna kukosa swali wala kuacha swali likikushinda na madaftari yanatakiwa mapema sana yakusanywe kabla somo halijaanza.
Lenyewe linakaa nje kwenye dawati linasahihisha na moustach wake mzito, pembeni ana kopo moja usawa wa kufika magotini lililojaa maji yaliyotapakaa pilipili na rundo la fimbo.
Ogopa hapo kila mtu darasani yupo kimya anajisomea mana kuongea kutasababisha kutembea kwa bakora baada ya kupata majina kutoka kwa wanahabari wake monitor na monitress lasivyo nao wasipotaja hayo majina kiama cha bakora kitawatembelea.wakati huo linapitia daftari moja baada ya lingine,( kila
Siku unapewa maswali kama50 hivi ukafanye nyumbani) na likishamaliza kupitia linakuita ukachukue daftari.
sasa omba usiwe umekosa swal kwani kila kosa moja unapata bakora moja umechafua au umekata lakini umepata swali bado utakula bakora moja kwa kila uchafu wako, sijui hujajaladia ni bakora tu,karatasi imechanika au umechana baada ya kuona umekosa mtatambuana pale.
Hiyo ndio ilikuwa tuishen zinazojenga nidhamu,umakini kwenye kufanya mambo yako na kutafakari kabla hujatenda, kwani tulikua makini sana kuhakikisha hatukosei wala kuchafua daftari Kwa kukata au kufuta, kwani matendo yote hayo yana adhabu na kutufanya na sisi tujitahid kwenda na standard za mwl wetu kwani ndiye anayetuelekeza namna ya kuwa bora.
na vilevile alinijengea mazoea ya kuweka kumbukumbu zangu za masomo. Nilipoanzia mpaka nilipoelekea( development process yangu).
Alikua mwl mzuri sana kwani wengi waliosoma kwake walikua wanafaulu mitihani ya darasa la 7
RIP MWALIMU NJOWOKA