Mwalimu jenga mahusiano bora na mwanafunzi wako

Mwalimu jenga mahusiano bora na mwanafunzi wako

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
f1c9e2fb459212fac754e7ab028b0980.jpg

Image Source: Pinterest

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa,
"Walimu wanaotanguliza uhusiano sio tu kuwa na wanafunzi kwa mwaka mmoja. Wana wanafunzi wanaowaona kama mwalimu wao wa Maisha"

Mateso tuliyopitia kwenye elimu yetu si lazima kizazi hiki kipitie.

Mateso yaliyofanya wengi kutokujiamini kutokana na kauli za walimu wao juu ya uwezo wao na mafanikio. Wanafunzi walio waona walimu kama maadui.

Hivyo mwalimu zingatia haya katika mawasiliano na mtoto au mwanafunzi wako ili kujenga mahusiano mazuri katika kuinu uwezo wake na taaluma.

1. Kuhusiana na hisia: Mwandishi anaelezea kuheshimiwa kwa hisia za watoto na anasema, Wakati unataka mtoto wako akuelewe, ni muhimu kwanza kukubali hisia zake.

Swali: Je, hisia ambazo hazijasikilizwa zinaenda wapi?
Ni yapi madhara yake kwa mtoto?

2. Kusikiliza kwa makini: kuna watoto wamepoteza kujiamini na hii ni kutokana na kutokusikiliza au kupuuzwa hivyo hili lina waathiri pale wanapotakiwa kutoa mawazo yap ila hawajiamini na mwandishi anasema, watoto wanahitaji kujiamini kuwa sauti zao zinaguswa na kusikizwa. Hii inawasaidia kujifunza kujieleza vema.

3. Kuepuka kukosoa moja kwa moja: Najua wewe mwenyewe umefanya kazi taasisi mbalimbali kna kukosolewa kuna umiza hasa pale ambapo hamna maelekezo ya kukujenga zaidi. Kwa mtoto mwandishi anasema hivi, badala ya kumlaumu, jaribu kueleza kile unachojisikia kuhusu kitendo chake.

Hili litamjenga kutafakari kitendo chake na hata hatua anaweza kufikiria jambo gani anaweza kufanya ili kurekebisha( he can recommend a solution for the problem he/ she caused.

3. Kutoa muongozo zaidi badala ya amri: Kwanza itamfanya afanye kwa heshima na kujiamini na mwandishi anasema hivi, badala ya kusema ‘fanya hivi’, jaribu kusema, ‘unafikiri ni hatua gani nzuri ya kuchukua.

4. Kujenga ushirikiano: Tunaishi kwenye jamii ambayo watoto wanashindwa kusema hata kile walichofanyiwa kwa wazazi kutoka na ukali wao na mwandishi anasema, kujenga mazingira ya ushirikiano kati ya mzazi na mtoto husimamia mahusiano bora na yanayoweza kudumu.
......
Kwa semina mbalimbali juu ya mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi nitafute inbox

Asante!!
 
Back
Top Bottom