Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Jina la Mwalimu Julius Nyerere linasomeka kwenye mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km)and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport,
Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region,Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopia kama mtu pekee duniani katika historia ya karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.
Mwalimu Julius Nyerere amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yoyote katika historia ya ukoloni barani Afrika, nchi hizo ni Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975 (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990
(Namibia) na 1994 (South Africa), Mwalimu Julius Nyerere ndiye kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hotuba yake maarufu akisema kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana, Mwalimu Julius Nyerere ndiye mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini- Anti Apartheid Movement mwaka 1959 pamoja na Trevor Huddleston nchini Uingereza.
Kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".
- Watanzania kwa namna ya pekee tunamkumbuka Mwalimu Julius Nyerere kwa kupigania Uhuru wa Taifa letu
Mwalimu Julius Nyerere alisimamia mali asili zetu,alisema kama hatuna uwezo wa kuchimba madini yetu yakawanufaisha watanzania basi tuyaache bila kuchimbwa hadi tutakapopata akili na uwezo wa kuyachimba kwa faida ya Watanzania, Mwalimu Julius Nyerere hakutaka wazungu watuibie madini yetu na rasilimali zinginezo, daima Mwalimu Nyerere alitanguliza maslahi ya Watanzania kuliko maslahi yake binafsi.
Je leo hii ni nani awezae kufanya kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere!? Mwalimu JuliusNyerere alitoa Elimu bure kwa watanzania kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, Mwalimu Julius Nyerere alijenga miundo mbinu ya reli, bandari na barabara. Mwalimu Julius Nyerere alianzisha mashirika ya Umma kama Air Tanzania, TRC, Tazara n.k Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na aibu kwa mafisadi wala wahujumu uchumi wa Taifa hili, aliwachapa viboko wakawaonyeshe wake zao,Mwalimu Julius Nyerere hakuwa tayari kutii maagizo ya mabeberu. Mwalimu Julius Nyerere ndiye mzalendo aliyekuwa tayari kufa kwa ajili ya Taifa la Tanzania, daima alitanguliza mbele masalahi ya Taifa la Tanzania, Maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere yalikuja kufanyika kazi na Rais John Pombe Magufuli, kuhamisha ofisi za Makao makuu ya Serikali toka Dar es Salaam hadi Dodoma na kujenga wizara zote za Serikali, kulijenga Bwawa la Rufiji kwa ajili ya kuzalisha Umeme wa megawat 2015 ambazo ni mara mbili ya hitaji la Taifa hivyo kuchochea uwekezaji wa viwanda ambavyo vingesaidia mnyoror wa thamani kwa malighafi na bidhaa za Tanzania.
Watanzania tunamuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa kutupatia uhuru, na ukombozi dhidi ya wakoloni kiasi kwamba tulimbatiza jina la Musa!, na kweli ikawa kama alivyo Musa, hakuweza kuwaingiza wana wa Israel kwenye ile nchi ya ahadi, aliishia njiani, ila Mungu akawaahidi wana Israel kuwaletea Mkombozi, Masiya, kuikamilisha ile kazi ya Musa!.
Je Mungu alimleta nani kuwa Mkombozi wa Watanzania baada ya Mwalimu Julius Nyerere? Watanzania wengi wanasema Magufuli ndiye yule masiya baada ya Mwalimu Julius Nyerere, yaani hatimaye Mungu ametukumbuka. Lakini kwa nini watu wanamtaja Hayati John Pombe Magufuli kama mtu aliyetembea kwenye njia ya Hayati Baba wa Taifa. Mwalimu Julius Nyerere, yapo mambo kadhaa yaliyofanya watu wamfananishe Rais Magufuli na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere !? Dhamira ya Hayati Rais John Magufuli kufufua mashirika ya umma, kukomesha wizi wa madini, kupitia upya mikataba ya madini, kuzuia hujuma ktk miradi ya umeme, kuhuisha reli ya kati na Tazara na ile ya Kilimanjaro, kununua meli mpya, vivuko na ndege, kukomesha ujangili wa tembo, kutumbua mafisadi, kukataa maagizo ya mabeberu na kurejesha heshima ya nchi,ni Faraja kwamba Matendo ya Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Rais John Magufuli ni fundisho kwetu kuwa wazalendo, wachapa kazi na kuutetea Uhuru na kulinda rasilimali za Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Taifa lake, katika hotuba nyingi za Rais Magufuli, alisisitiza kwamba amejitoa mhanga kwa ajili ya watanzania, alisimamia alichokiamini,alikemea mabeberu weupe na vibaraka wao, alikubali kufa kishujaa kuliko kusalimu amri, alisisitiza, tutamkumbuka kwa wema na kweli tumeanza kumkumbuka na tunaendelea kumkumbuka.
Nimalizie kwa kusema, wakati sahihi hakuna watu sahihi, tunapopata mtu sahihi uonekana hayuko sahihi, hii inamaanisha ujinga bado umetujaa kuweza kukumbatia maradhi na umasikini, ulipoondoka Mwalimu ule ukoloni mamboleo ukatawala, uliacha ubinafsishaji,ukaja ufisadi na sasa kuna uchawa hadi kwa wazungu, alikuja mtu unayefanana nae kwa kiasi fulani lakini hakukaa sana akaondoka, kwa kiasi fulani bila unafiki na mihemko ya kisiasa, mtu huyo ni Hayati Rais John Pombe Magufuli,yale ambayo kila mtanzania alitamani kumuona kiongozi mkuu wa nchi anayafanya John Pombe Magufuli aliyafanya, tulishuhudia akitamka waziwazi kwamba kwenye mambo mengi tunapigwa, jambo ambalo hakuna mtanzania aliyebisha, alienda mbali zaidi na kutuonyesha namna ambavyo wapigaji wanatupiga, jambo ambalo ukiacha wewe Mwalimu Julius Nyerere hakuna mkuu mwingine aliyetunasua,Hayati Rais John Pombe Magufuli aliwaumbua majizi, matapeli mitaani, mavishoka, watu ambao waliishi kutegemea akili chafu za waliowazaa, hivi leo wengi wanamkashifu lakini ni wale wezi, matapeli, waliogushi vyeti, na wale walioishi maisha ya ujanjaujanja, Magufuli akaja kuikata mirija yao, huyu ndio alitembea kwenye njia zako hata watu kumfananisha na wewe, kama ulivyokuwa wewe Mwalimu Nyerere basi Hayati Rais Magufuli aliithamini nguvu ya Umma kwa kuwaonya watendaji hadharani ili wajihadhari nayo, alipobaini hawamwelewi, aliwageuka watendaji na kuunga mkono madai ya Wananchi dhidi ya watendaji, rudi tena japo mara moja Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,
Ahsante kwa ajili ya maisha yako. Ahsante kwa ajili ya maisha ya kijana wako, Hayati Benjamini William Mkapa, ahsante kwa ajili ya maisha ya mfuasi wako Hayati Rais John Pombe Magufuli,
Usiku mwema.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.