Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mwalimu Nyerere alikuwa, ''brilliant orator,'' na akikijua Kiingereza vyema.
Nimesoma barua zake katika Nyaraka za Sykes na kuna hii moja niliyoipenda sana ya 1954 mwezi mmoja baada ya TANU kuundwa.
Naweka kipande cha nukuu ya barua hiyo hapi chini kabisa.
"The Central Committee of the Party submitted its memorandum to the visiting mission as was the tradition in those days.
TANU pointed out in its memorandum that to the Africans of Tanganyika the most important issue to them was to resolve the Meru Land case peacefully.
The gravity of the matter and the seriousness with which TANU was to confront the government can be felt in the tone of the memorandum said to be authored by Nyerere, Abdulwahid, Stephen Mhando and Earl Seaton.
The legal language of Seaton is evident in the following passage:
"We realise the apparent incompatibility between the implementation of the resolution and imperial prestige. But to us this is not a matter of prestige, it is both a matter of high principle and of bread and butter. As far as this Union is concerned an important principle has been violated and we will not rest until it has been put right." (TANU memorandum to the United Nations Visiting Mission, 24th August, 1954, Sykes’ Papers).
Mwalimu Nyerere na Earle Seaton baada ya uhuru
In Shaa Allah nitaekeza hapa Majlis yaliyopitika jana yake kabla Mwalimu Nyerere hajafanya hii press conference kuhusu UDI 1965.
Ahmed Rashad Ali akiwa Deputy Permanent Secretary Information alikwenda nyumbani kwa Mwalimu Msasani kutaka kumsikiliza kuhusu Ian Smith.
Akamkuta pamoja na Mwalimu Dossa Aziz na Lucy Lameck na Mwalimu alikuwa kamaliza matayarisho yake kuhusu mkutano huu na waandishi wa habari siku ya pili yake.
Hii ndiyo siku Mwalimu alimweleza Ahmed Rashad kile alichokiita "The TANU Spirit."
Kwanza ningependa kueleza kuwa Ahmed Rashad na Mwalimu Nyerere wakijuana vyema kabisa.
Ahmed Rashad alikuwa rafiki wa Abdul Sykes toka mwaka wa 1939 wote wakiwa watoto wadogo.
Abdul alikuwa kafuatana na mjomba wake Omar Amirani kwenye jengo la Arab Association Ring Street (sasa Mtaa wa Jamhuri).
Ilikuwa katika sherehe za Pasaka wakati Wazanzibari wamekuja Dar es Salaam kwenye, ‘’Sports.’’
Mwaka ule ilikuwa zamu ya Zanzibar kuja Dar es Salaam kwani mwaka uliopita watu wa Dar es Salaam walikuwa wamekwenda Zanzibar.
Huyu Omar Amirani ni mtoto wa Bi. Msiki Simlaleo mdogo wake Bi, Mruguru bint Mussa mama yake Abdul Sykes.
Bi. Miski aliolewa na kijana wa Kiarabu, Amirani na kuzaliwa Omar na hivi ndivyo Omar alivyopata kuwa mwanachama wa Arab Association na si African Association chama cha Kleist mume wa mama yake mkubwa.
Bi. Miski ni katika ukoo wa Chief Mkwawa na alitokea Iringa akaja Dar es Salaam kwa dada yake mke wa Kleist Sykes na hivi ndivyo alivyokuja kuolewa na kijana wa Kiarabu Amirani.
Ahmed Rashad yeye mama yake alikuwahi kuolewa na Sultan Sayyid Ali bin Humud.
Sayyid bin Humud mama yake alikuwa Mnyasa.
Ahmed Rashad mama yake akiitwa Bi. Ruzuna bint Tamim lakini jina lake maarufu lilikuwa
Mame Bwana.
Rashad na yeye pia alikuwa amekuja pale Arab Association na mjomba wake.
Hivi ndivyo Abdul na Rashad walivyokuja kufahamiana na urafiki wao ukadumu hadi Abdul alipofariki mwaka wa 1968.
Kwa ajili hii Ahmed Rashad kajua mengi kuhusu Nyerere kupitia kimywa cha Abdul Sykes mtu aliyempokea Nyerere Dar es Salaam mwaks wab1952 na wakafanya mengi pamoja katika kuunda TANU.
Mwalimu Nyerere amemjua Ahmed Rashad kwa mchango wake katika ukombozi wa nchi za Afrika wakati alipokuwa mtangazaji wa Radio Free Africa Cairo miaka ya 1950 ambako alikuwa akitangaza na matangazo ya radio hii yalikuwa yanapendwa sana na wasikilizaji Waafrika Afrika ya Mashariki yote hasa Zanzibar na Tanganyika.
Rashad katika matangazo yake akiwatukana wakoloni wote, Waingereza na Wareno akiwaita, ‘’Majibwa Meupe.’’
Mapinduzi ya Zanzibar yalimkuta Rashad bado yuko Cairo na alimuunga mkono Karume na ASP.
Swali la kwanza Ahmed Rashad alilomuuliza Mwalimu Nyerere ni kama Waingereza watapeleka jeshi kumtoa Ian Smith madarakani.
Nyerere alijibu kuwa mlowezi Ian Smith na Waingereza ni mtu na mjomba wake, Waingereza hawatafanya lolote kumtoa Ian Smith Rhodesia.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi na Mwalimu ndipo alipomwambia Rashad kuwa anataka kumueleza hali ilivyokuwa Tanganyika wakati wa kupigania uhuru.
Ndipo Mwalimu Nyerere akamueleza Ahmed Rashad wema na ukarimu wa Mzee Mshume Kiyate kwake.
Mwalimu alimweleza Ahmed Rashad kuwa wakati anaishi Magomeni katika miaka ya 1950 iko siku ametoka nyumbani kwenda sokoni Kariakoo kuhemea chakula lakini alikuwa hana hata senti moja mfukoni.
Nyerere alikuwa anatembea kwa miguu na alipofika makutano ya Morogoro Road na Cameron Road (sasa United Nations) akakutana na Mzee Mshume Kiyate.
Mzee Mshume akamuuliza Nyerere wapi alikuwa anakwenda.
Mwalimu akamwambia kuwa alikuwa anakwenda sokoni lakini alikuwa hana hata senti moja mfukoni.
Mzee Mshume aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake akatoa noti ya shilingi mia akampa Nyerere.
(Ukitaka kujua thamani ya fedha hizi ni kuwa nyumba nzima Kariakoo ilikuwa inauzwa kwa shs: 200.00).
Siku ya pili katika kikao cha Baraza la Wazee wa TANU Mzee Mshume akasema kuwa si haki kumpa Nyerere kazi mbili.
Apambane na Twining na ahemee chakula cha wanae.
Mzee Mshume akasema kuwa kuanzia sasa yeye atashughulikia chakula cha Mwalimu Nyerere ili abaki na kazi moja tu ya kuongoza mapambano dhidi ya Waingereza.
Mzee Mshule alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.
Kila asubuhi Landrover ya TANU ikiendeshwa na Said Kamtawa ilikuwa ikionekana sokoni Kariakoo ikichukua vikapu vya mahitaji ya siku ya nyumba ya Mwalimu Nyerere.
Ulipopatikana uhuru Mwalimu akamwambia Mzee Mshume kuwa hapana haja tena ya kumpelekea vikapu vya vyakula kwa kuwa sasa analishwa na serikali.
Mzee Mshume hakukubali akamwambia Nyerere kuwa chakula anachopewa na serikali hicho awape wageni wake lakini yeye na wanae wale chakula kile anacholeta yeye.
Mwalimu akamaliza kwa kumwambia Ahmed Rashad, ‘’This was the TANU spirit.’’