Mwalimu kutumikia kifungo cha maisha mara mbili na miaka 30 jela kwa kulawiti mwanafunzi

Mwalimu kutumikia kifungo cha maisha mara mbili na miaka 30 jela kwa kulawiti mwanafunzi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma mkoani Mara, imemuhukumu kifungo cha maisha jela mwalimu Idrisa Athumani (29) wa shule ya Msingi Kyawazaru iliyopo wilayani Butiama baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake (14).

Hukumu hivo iliyotolewa leo ljumaa Septemba 23, 2022 ni ya tatu kutolewa dhidi ya mwalimu huyo ambapo hukumu ya kwanza ilitolewa Septemba 14, mwaka huu na Mahakama ya Wilaya ya Musoma mwalimu huyo alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mara mbili mwanafunzi wake mwingine.

Hukumu ya pili ilitolewa Septemba 16, 2022 na Mahakama hiyo hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti wanafunzi wake mwingine (12).

Hukumu ya tatu imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo dhidi ya mashataka yaliyokuwa yakimkabili mwalimu Athumani.

Chanzo: Mwananchi

Hukumu nyingine: Mwalimu afungwa miaka 30 kwa kumlawiti mtoto
 
Kwahyo jamaaa sasa hivi kashalala na gwanda lake anasubiri uji asubuhi daaaah
 
Angalau Ajira moja ipo wazi haya changamkieni
 
Back
Top Bottom